Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KESI YA PINDA KUUNGURUMA TENA LEO MAHAKAMA KUU

KESI YA PINDA KUUNGURUMA TENA LEO MAHAKAMA KUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya kikatiba inayomkabili Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , iliyofunguliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai Pinda alivunja Katiba kutokana na kauli aliyoitoa Bungeni, akiagiza vyombo vya dola kuwapiga wale ambao watakaidi kutii sheria zinazotolewa na vyombo husika. Walalamikaji wanadai kuwa amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga wananchi ni kinyume na katiba.
Hata hivyo, Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) aliyeunganishwa katika kesi hiyo waliweka pingamizi la awali, pamoja na mambo mengine wakidai kuwa walalamikaji na watu walioorodheshwa katika kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kumfungulia kesi.
Kabla ya kesi hiyo kuahirishwa, mwaka jana, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG), George Masaju, aliieleza Mahakama Kuu kuwa kesi ya kikatiba inayomkabili Waziri Mkuu, Pinda ni batili, hivyo inapaswa kufutwa.
Masaju, alisema hayo wakati alipokuwa akiwasilisha pingamizi la awali la Pinda ,ambapo alisema sheria zinamlinda Waziri Mkuu kutoshtakiwa wala kuhojiwa na chombo chochote juu ya kauli aliyoitoa Bungeni.
Katika pingamizi hilo, DAG Masaju alidai kesi hiyo ni batili na iko mahakamani isivyo halali kwa kuwa inakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Sheria ya Mamlaka, Kinga na Haki za Wabunge ya mwaka 1988. Akifafanua hoja hizo, DAG Masaju alisema Pinda analindwa na Katiba Ibara ya 100 (1) na (2)
Akinukuu ibara hizo, alisema ibara ya kwanza inaeleza kuwa kutakuwa na uhuru wa mawazo na majadiliano bungeni, ambao hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote, au katika mahakama yoyote nchini.
Ibara ya pili inaeleza kuwa mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kwa jambo lolote alilosema, au alilolitenda, au alililoliwasilisha bungeni kwa njia ya maombi, mswada, hoja au vinginevyo. “Msingi wa shauri hili unatokana na jambo lililosemwa Bungeni na mmoja wa wabunge wakati wa shughuli za bunge.”
Kwa upande wake Wakili wa Serikali, Gabriel Mlata, alisema kesi hiyo ni batili kuwepo mahakamani kwa kuwa walioifungua wamekiuka utaratibu wa uwasilishaji wa mashauri kama hayo kwa mujibu wa amri na kanuni za uendeshaji wa mashauri ya madai.

Chanzo:Majira

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa