Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa
13 wanaodaiwa kuhusika katika tukio la ujambazi uliofanyika katika
Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni hivi karibuni ambapo kiasi cha sh.
390,220,000, dola 55,000, euro 2,150 na vitabu vya hudi 50 viliibwa.
Miongoni
mwa wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni wanawake wawili ambao ni mameneja
wa Barclays, tawi la Kinondoni ulipofanyika wizi huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar
es Salaam, Suleiman Kova, aliwataka mameneja wa tawi hilo wanaoshikiliwa
Alune Kasililika (28) na mwenzake ambaye ni Meneja Uendeshaji, Neema
Bandari.
Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa ni Frederick Lazaro (19),
Kakamiye Julius (31), Idd Nguvu (32)Sazery Osward, Boniface Ndaro
(29)na Erasimus Berbard (38).
Kamanda Kova aliwataja wengine kuwa ni
Deo Isdory (32), Mohamed Athuman (31) Licy Amos (30) na Grace Amon
(39).Alisema tukio hilo lilifanyika Aprili 15 mwaka huu saa tatu na nusu
asubuhi katika tawi la Kinondoni.
Alisema siku ya tukio watu waliokuwa na silaha aina ya SMG na Bastola waliingia ndani ya benki na kupora kiasi hicho cha fedha.
Kamanda
Kova, alisema baada ya kutokea wizi huo Jeshi la Polisi liliuda kikosi
maalum cha upelelezi (Task Force) na kugundua kwamba robo tatu ya fedha
zote zilizoibwa zilichukuliwa kabla ya siku ya tukio la ujambazi huo.
Alisema
kuwa majambazi hao walifika eneo la tukio na kuwatishia kwa silaha
watumishi wa benki hiyo na kuwaweka chini ya ulinzi na hatimaye kutoroka
na pesa hizo kwa kutumia pikipiki aina ya Fekon.
Kamanda alisema
kuwa Jeshi la Polisi limegundua kuwa wizi huo unaohusisha mabenki
umekuwa ukihusisha wafanyakazi wenyewe pamoja na mameneja wao
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment