Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali,Ludovick Utouh (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ofisi za Bunge mjini Dodoma jana �wakati akitoa �ripoti ya
�mapato na matumzi ya serikali.PICHA:TRYPHONE MWEJI
Alisema hayo jana wakati akizungumzia ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013. Utouh anasema Tanzania ina magereza 122 yenye uwezo wa kuchukua wafungwa 22,669, lakini kwa sasa yanatoa huduma kwa wafungwa 45,000, kiwango alichosema ni kikubwa na kinachohatarisha usalama wa wafungwa hao.
“Kutokana na ongezeko hilo limechangia ugumu wa kudhibiti na kufuatilia haki za wafungwa kwenye magereza yenye msongamano mkubwa,” alisema.Pamoja na idadi kubwa wa wafungwa, lakini Idara ya Magereza imekuwa ikipata bajeti finyu tofauti na inayopendekezwa, hali inayowafanya watumia njia nyingine za kupata fedha za kuwatunza wafungwa hao.
Alisema hali hiyo inachangia kuvuruga wakati mwingine bajeti kuu kwa fedha zilizopangwa kufanya shughuli nyingine na kuchukuliwa kwa ajili ya kuihudumia idara hiyo.
Alisema kwa mfano bajeti ya 2012/13 idara hiyo iliomba Sh. bilioni 131.5 kwa matumizi ya kawaida na Sh. bilioni 51.60 kwa miradi ya maendeleo, lakini walipewa bajeti yenye ukomo wa Sh. Bilioni 51.4 kwa matumizi ya kawaida na Sh. bilioni 1.3 kwa shughuli za maendeleo.
Alisema baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ukomo wa bajeti hiyo ni chakula cha wafungwa ambacho kilipangiwa Sh. bilioni 32.4 na bajeti iliyoidhinishwa ni Sh. bilioni 8.
Utouh alisema kwa upande wa mavazi ya wafungwa, bajeti halisi ilikuwa ni Sh. bilioni 1.6, lakini kilichoidhinishwa ni Sh. bilioni 0.5.
Kwa upande wa sare za askari alisema bajeti halisi ilikuwa Sh. bilioni 3.7, lakini iliyoidhinishwa ni Sh. bilioni 0.35. Utouh alitoa mapendekezo kuwa kutokana na changamoto zinazoikabili Idara ya Magereza ni vema Mahakama ya Tanzania ikaharakisha kutoa maamuzi ya kesi zilizopo kwani kwa sasa kuna idadi kubwa ya mahabusu magerezani wanaosubiri kusikilizwa kesi zao.
Alipendekeza pia kwamba serikali iiwezeshe Idara ya Mahakama iwe na uwezo wa kufanya kazi zake kikatiba kwa kuipatia fedha, nyenzo na watumishi wenye sifa na idadi inayoendana na majukumu yake.
“Ili kupunguza msongamano katika magereza na gharama za kuwahudumia wafungwa, Mahakama inashauriwa kutoa adhabu mbadala kwa makosa madogo,” alisema.
Serikali imeshauriwa pia kubuni miradi ya upanuzi wa miundombinu ya magerezaikiwa ni pamoja na kujenga magereza mapya na kukarabati yaliyopo ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za kuwalisha wafungwa na kuwavisha na kuwatibu na kuwapatia haki zao za msingi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment