awataka wabunge wengine wasije Dar es Salaam, wakae kwenye majimbo yao
Mbunge wa Ilala, Hassan Musa ‘Zungu’
Na Damas Makangale, Moblog Tanzania
MBUNGE wa Ilala, Musa Hassan
maarufu kama ‘Zungu’ leo asubuhi katika kikao cha Bunge la Bajeti
kinachoendelea mjini Dodoma amekataa kuunga mkono Bajeti ya ofisi ya
Waziri Mkuu yenye makadirio ya kiasi cha shilingi trilioni tano.
Akizungumza kwenye kipindi
cha maswali na majibu ya ofisi ya Waziri Mkuu Bajeti ya 2014/2015,
Mbunge Musa Hassan ‘Zungu’ amesema kwamba hataunga mkono bajeti ya ofisi
hiyo kwa sababu haina kipaumbele kwa mkoa wa Dar es Salaam katika
maswala ya miundombinu, kitengo cha maafa na maji.
“Mheshimiwa Naibu wa Spika
kwa kweli siungi mkono bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kama mambo kadhaa
kama ya miundombinu, maji na utendaji mbovu wa baadhi ya wakurugenzi wa
jiji kutumia madaraka vibaya na kuwaumiza wananchi ambao ni wapiga kura
wetu,” amesema Zungu
Aliongeza kwa kusema kwamba
kuna baadhi ya wabunge wamepiga kelele Dar es Salaam inapendelewa wakati
miundombinu ya jiji hilo ni mibovu na wananchi wanateseka na mafuriko
katika maeneo kadhaa bila msaada wa serikali.
“Na nyinyi wabunge mnaosema
kwamba Dar tunapendelewa msije kabisa mkae huko mlipochaguliwa na wapiga
kura wenu tusiwaone Dar es Salaam,” amesema Zungu huku akishangiliwa na
baadhi ya wabunge
Zungu amesema kuwa katika
Mkoa wa Dar es Salaam kuna baadhi ya watendaji hasa wakurugenzi
wanajiamulia mambo na kuchukua ushuru katika sehemu mbalimbali huku
wakisumbua wamachinga, boda boda na mama ntilie kwamba kuna sehemu ni
smart areas.
Amesema kwamba hakuna smart
areas kama sehemu kubwa la jiji kuna matope na barabara ni mbovu na
kuzuia wafanyabiashara ndogo ndogo kushidwa kujitafutia riziki na
kuendesha maisha yao ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment