MABAO
2-0 waliyopata Nigeria dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ya vijana
chini ya umri wa miaka 20,Ngorongoro Heroes jioni hii uwanja wa taifa
katika Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa
vijana yamempa kazi ngumu kocha mkuu John Simkoko kusonga mbele.
Ngorongora
walipata nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha kwanza, lakini bado
ugonjwa wa kutotumia nafasi muhimu unazidi kuitafuna timu hii.
Mshambuliaji Saady Kipanga alishindwa kuonesha makeke yake baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Mpaka
dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika milango ya timu zote
ilikuwa migumu, huku kipa namba moja wa Heroes, Aishi Manula akiumia.
Kipindi cha pili, Manula alishindwa kurejea uwanjani na kumpisha kipa namba mbili, Peter Manyika.
Katika
Kipindi hicho cha pili Ngorongoro waliingia kizembe na kujikuta
wakifungwa mabao mawili na kumaliza mechi kwa kipigo cha nyumbani cha
mabao mawili kwa sifuri.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment