Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

kijana ambaye ni kibaka ameshikilia pikipiki waliyo tumia kufanyia uhalifu

kipigo kikali mtaloni na kuona haka kadaraja ni sehemu ya kujistili


vijana wawili ambao ni vibaka wamejeruhiwa vibaya na kunusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kali kuwaachia kichapo ambapo kipigo hicho kimewafikia baada ya vijana hao kumvamia dada mmoja aliyekuwa akitokea bank ya acces maeneo ya kijitonyama jijini dar na kuweza kumpora begi dogo alilo kuwa ameweka vitu vyake
baada ya vijana hao kufanya uharifu huo ambapo walikuwa na usafiri wa pikipiki walianza kuondoka kwa kukimbiza pikipiki hiyo ndipo msamalia mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake aliamua kuchukua gari lake aina ya toyota carina na kuweza kuwakimbiza na kuigonga kwa nyuma pikipiki hiyo na vijana hao kuweza kuanguka na kukamatwa ndipo walipo anza kuwa kugawiwa zawadi za kazi yao
hatimaye maisha yao kuokolewa na vyombo vya usalama vilipoweza kufika na kuwasaidia vibaka hao wakiwa hoi na kuweza kunusurika na kifo
0 comments:
Post a Comment