Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi, ni mmoja wa watoa mada katika semina hiyo.
Mfuko
wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) utaendesha Semina ya mafunzo ya siku 3
kwa Wanawake Wajasiriamali itakayofanyika kuanzia tarehe 23 hadi tarehe
25 Juni 2014, kuanzia saa 2 asubuhi katika ukumbi wa JKT Mgulani,
Temeke,jijini Dar es salaam.
Lengo
la mafunzo haya kwa mwaka huu ni kuwaelimisha wanawake jinsi ya kupata
mitaji kwa ajili ya biashara, masoko pamoja na stadi za ujasiriamari.
Katika
semina hii mada kuu zitahusu Uwekezaji na Ukuzaji mtaji, Utunzaji wa
Kumbukumbu za Biashara kwa Kutumia Mashine za EFD, Kuwaunganisha
Wazalishaji na Masoko, Mbinu za kushiriki Maonesho ya Biashara, Utaalamu
wa kusindika Mazao, Usajili na Matumizi ya “Bar Code” na nyinginezo.
Aidha,
elimu juu ya maradhi sugu yanayorudisha nyuma maendeleo ya wanawake
itatolewa na jinsi ya kujikinga dhidi ya Malaria, Dengue, Saratani ya
Matiti na Shingo ya Uzazi pamoja na Fistula.
Watoa
mada katika semina hii ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Dkt.
Reginald Mengi, Wakufunzi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Soko la
Hisa la Dar-es-salaam- DSE, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara-TanTrade
na Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Pia kutakuwa na Madaktari kutoka Manispaa za Ilala na Temeke, hospitali ya Ocean Road na CCBRT.
Natumia fursa hii adimu kuhamasisha wanawake kuudhuria Semina hii muhimu
yenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake na vijana wajasiriamali na
kuwainua kiuchumi kwa siku zote 3 kuanzia tarehe 23 hadi 25, Juni 2014.
Hakuna malipo kwa washiriki
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Ndugu, Stephen Emmanuel
20/06/2014
0 comments:
Post a Comment