Home » » BOT YATOA HADHARA KUMILIKI FEDHA BANDIA

BOT YATOA HADHARA KUMILIKI FEDHA BANDIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa hadhari kwa wananchi kutambua kuwa kughushi pamoja na kumiliki fedha bandia kwa nia ya kuzitumia ni kosa la jinai, linalosababisha mhusika kushtakiwa kwenye vyombo vya sheria.

Imegundulika kwamba kukosekana elimu kuhusu utunzaji wa noti, kunasababisha kuwepo uchakavu wa noti hizo katika mzunguko wa fedha hali inayochangia kushuka uchumi nchini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa benki hiyo Idara Kurugenzi za Kibenki, Patrick Fata alisema wanatoa elimu kwa wananchi ili kuweza kutunza na kuzihifadhi vyema noti hizo ili kuepusha uchakavu unaohatarisha kushusha hali ya kiuchumi nchini.

Alisema hali ya uchumi inashuka kutokana na gharama kubwa wanazotumia kutengenezea noti nyingine, ili kuziingiza katika mzunguko wa fedha pindi noti zilizokuwepo kuonekana chakavu, kutokana na utunzaji mbaya wa noti hizo.

"Changamoto kubwa tunayukumbana nayo ni juu ya utoaji wa elimu, huku tukiwa na matumaini elimu yetu iifikie jamii kuhusu utunzaji wa noti zetu, kwa sababu unavyochakaza noti, inabidi tuchapishe nyingine hali inayosababisha kutumia gharama kubwa kutengeneza noti nyingine na hapo ndipo hali ya uchumi inapokuwa katika wasiwasi wa kushuka kulingana na gharama kubwa inayotumika kutengeneza noti hizo," alisema Fata.

Alisema wanatumia nafasi hiyo ya viwanja hivyo vya maonesho ya Sabasaba, kutoa elimu kwa jamii kuhusu uhifadhi na kutunza noti hizo ili kuepuka uchakavu unaojitokeza kwenye matumizi ya noti.

Fata alisema mbali na kuwepo na changamoto za noti chakavu, pia uwepo wa matumizi ya noti bandia ni moja ya changamoto zinazoikabili benki hiyo hapa nchini.

Pamoja na hayo, Fata alisema ili kuendelea kupambana na uchakavu wa noti unaoendelea kujitokeza BoT, inatarajia kuingiza katika matumizi sarafu ya 500 mwezi huu ikienda sambamba na kipindi hiki cha mwaka wa fedha.

Alisema sarafu hizo za 500, zinatarajia kuanza kuingia katika matumizi mwezi huu huku ikitarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20,zikiwa na ubora wake huo huo

 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa