Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaad Musa Salum.
Amesema Uislamu kuhusishwa na matukio ya uhalifu yaliyotokea Arusha na Zanzibar siku za karibuni siyo sawa, kwani dini hiyo inaheshimu haki za binadamu na kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani kama dini nyingine.
Alisema hayo katika semina ya pili ya masheikh na maimamu iliyowashirikisha mabalozi wa nchi mbalimbali duniani na viongozi wa dini nyingine, kwa lengo la kupinga dhuluma na udhalimu wa ardhi wanayofanyiwa Wapalestina.
“Tunapinga vikali vitendo vinavyoendelea. Vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu kuwabaini wahalifu na kuwachukulia hatua. Pia kama waislamu na dini nyingine tunaungana kukemea vitendo hivi bila kuvihusisha na imani yoyote. Pamoja na kuwaombea wenzetu Wapalestina wawe na uvumilivu na kuendelea kudumisha amani,” alisema Sheikh Alhaad.
Aliwataka waislam Wapalestina kuwa na moyo wa utulivu na amani katika kipindi wanachopitia cha dhuluma na uonevu katika ardhi yao.
“Kama waislam duniani kote, tunapinga na kuwaombea Wapalestina wawe na moyo wa uvumilivu na kudumisha amani kama tuliyonayo sisi Watanzania na kumtukuza Mwenyezi Mungu katika wakati mgumu wanaopita,” alisema Sheikh Alhaad.
Alisema kila Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imeteuliwa kuwa siku ya “Qudsi” ambayo lengo lake ni kukumbuka mwaka, ambao Wapalestina walinyang’anywa ardhi yao.
Naye Imamu wa Msikiti wa Masjid Ghadir Kigogo, Hemedi Jalala, alisema yanayoendelea Palestina nchi zote zinapaswa kusimama na kukemea ili wawe na amani na kwamba ni wajibu wa kila muislamu kukemea na kuichukia dhuluma na kudumisha amani ya nchi yake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment