Home » » SHULE ZAPIGANA VIKUMBO KUPANDA NA KUSHUKA

SHULE ZAPIGANA VIKUMBO KUPANDA NA KUSHUKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2014 yaliyotangazwa juzi yameonyesha kupiga hatua kwa baadhi ya shule na nyingine maarufu zikiporomoka.
Kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, akitangaza matokeo hayo juzi jijini Dar es Salaam, alisema asilimia 95.98 ya watahiniwa 40,695 waliofanya mtihani Mei mwaka huu, wamefaulu.
Kwa mujibu wa kitabu cha takwimu kilichotolewa na Necta, shule 100 kati ya 268 zilizosajiliwa kufanya mtihani Mei mwaka huu zenye watahiniwa zaidi ya 100, si shule za ufundi au zile maarufu zilizoingia katika kinyang’anyiro hicho.
Shule zilizoshuka
Baadhi ya shule zimeporomoka ikiwemo Marian Girls iliyokuwa nafasi ya kwanza mwaka jana hadi nafasi ya tano. Nyingine ni St. Mary’s Mazinde Juu (6 hadi 28), Ilboru (4 hadi 32) na Tabora Boys kutoka nafasi ya 15 hadi 36.
Shule nyingine ni Tabora Girls (7 hadi 41), St. Mary Goreti (25 hadi 54), Magufuli (30 hadi 55), Matema Beach (33 hadi 77), Shambalai (26 hadi 79), Shaaban Robert (38 hadi 87), Selesian (18 hadi 98) na Loyola kutoka nafasi ya 55 hadi 99.
Miongoni mwa zilizoporomoka zimo Masasi Girls kutoka 37 hadi 107, Rosmini (21 hadi 109), Tusiime (77 hadi 116), Uru Seminary (11 hadi 117), St. Peter Seminary (9 hadi 119), Kifungilo Girls (10 hadi 125), Consolata Seminary (65 hadi 130), Mafinga Seminary (59 hadi 155), Kibosho Girls (80 hadi 157), Mpanda Girls (64 hadi 160) na Lindi kutoka 91 hadi 177.
Nyingine ni Tegeta (58 hadi 179), Biharamulo (58 hadi 184), Usa Seminary (54 hadi 187), Ileje (98 hadi 202), Minaki (146 hadi 230) na Magu (kutoka 190 hadi 249).
Shule kumi za mwisho ni Ben Bella (kutoka 308 hadi 268), Fidel Castro (312 hadi 267), Tambaza (317 hadi 266), Muheza (301 hadi 265), Mazizini (328 hadi 264), Mtwara Technical (305 hadi 263), Iyunga Tecnical (294 hadi 262), Al-Falaah Muslim (114 hadi 261), Kaliua (252 hadi 260) na Osward Mang’ombe (kutoka 323 hadi 259).
Shule zilizopanda
Katika matokeo hayo shule zilizopanda zenye wanafunzi zaidi ya 30 ikilinganishwa na mwaka 2013 ni Igowole (kutoka 8 hadi 1), Iwawa (75 hadi 4), Nangwa (28 hadi 7), Uwata (24 hadi 8), Kibondo (27 hadi 9), Kawawa (24 hadi 10), Vwawa (39 hadi 11), Lufilyo (48 hadi 13) na Nyarubada (kutoka 204 hadi 14).
Nyingine zilizofanya vizuri ni Mwalimu J K Nyerere (kutoka 173 hadi 17 ), Mati (111 hadi 20), Changarawe (105 hadi 24), Chief Ihunyo (127 hadi 25), Usangi (88 hadi 27), J.J. Mungai (103 hadi 30), Dakawa (113 hai 31), Mwembeni (195 hadi 34) na Sekondari ya Namabengo kutoka 94 hadi 39
Sekondari ya Mwembetogwa imepanda kutoka 185 hadi 46, Cornerstone Leadership (112 hadi 47), Marangu (147 hadi 48), Kigwe (124 hadi 51), Mpwapwa (203 hadi 52), Singe (130 hadi 53), Mwinyi (151 hadi 56), Itigi (100 hadi 59), Midlands (166 hadi 64), Ocean (211 hadi 67) Sumve (179 hadi 71), Zanaki (212 hadi 85) na Utaani (kutoka 273 hadi 81).
Zilizofunga ukurasa kwa kuingia shule 100 ni Irkisongo (kutoka 242 hadi 91), Makumira (220 hadi 93), Eagles (278 hadi 96) na Sekondari ya Umbwe iliyopanda kwa nafasi tisa kutoka 106 hadi 97
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa