Na
Dismas Lyassa
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Salaam
Wapendwa
ndugu zangu wana habari…Asalam Aleikum…Tumsifu Yesu Kristo… Bwana Yesu
Asifiwe…!
Shukrani
Ndugu
wanahabari
Nawapenda
kuwashukuru kwa ujio wenu. Nichukue fursa hii niwatambulishe walioko mbele yenu
ili kufahamiana. Nianze kwa kujitambulisha mimi mwenyewe, naitwa Dismas Lyassa,
ni mwandishi wa habari mwenzenu…nimekuwa katika hii kazi kwa miaka 20 sasa na
nimewahi kufanyia kazi katika magazeti mbalimbali yakiwamo Alasiri, Financial
Times, Leo ni Leo na tangu 2005 nimekuwa nikifanyia kazi katika gazeti la
Mwananchi hadi sasa nikiwa mhariri anayeshughulikia masuala ya biashara na
uchumi. Pia toka mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa COTWU tawi la
Mwananchi Communications Limited, nafasi ambayo kisheria mtu anapaswa kudumu
kwa miaka mitano, lakini akitaka anaweza kugombea.
Utambulisho
Ndugu
wanahabari
Wengine
niliombatana nao ni mke wangu Mchungaji Rightess Lyassa wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Kawe -Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU) kanda ya Dar es Salaam,
wakili wangu Jebra Kambole kutoka kampuni ya Uwakili ya Law Guards ya Jijini
Dar es Salaam, na meneja kampeni Khamis Tembo.
Ndugu
wanahabari
Lengo
hasa la kuwaiteni mahali hapa ni kutoa taarifa kwenu kuwa ninagombea Urais wa
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania, uchaguzi ambao unatarajiwa
kufanyika Agosti 4-5, Dodoma.
Vipaumbele
vyangu ni vyangu
Ndugu
wanahabari
Nina
malengo ya kuifufua na kuleta TUCTA yenye uhai na mabadiliko ya kweli kwa
kufanya yafuatayo;
Ndugu
wanahabari
1.
Kupigania na kulinda haki za wafanyakazi;
Katika
kipaumbele hili lengo hasa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi yakiwamo-:
i.
Kulipwa
ujira/mishahara duni isiyoendana na uhalisia wa maisha.
ii.
Ucheleweshaji
wa upatikanaji wa ujira/mishahara
iii. Ucheleweshaji
fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya/ kiwango kidogo cha fedha za kujikimu
iv. Uhaba au
kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya
v.
Rushwa na
kuajiri kwa misingi ya kujuana kwa mfano katika Halmashauri ya Siha, wilaya
ambayo imegawanywa kutoka Hai, kuna pori kubwa la West Kilimanjaro mlimani
kabisa, hakuna maendeleo…ni suala la kawaida kuona watu wakiongea kilugha
ofisini kama lugha ya Taifa
vi. Wakubwa yaani
mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha wafanyakazi kwa kadri wanavyotaka wao,
sivyo inavyosema sheria.
vii. Uwepo wa mpangilio
usio sawa wa ujira/mishahara.
viii. Kutopewa posho au kupewa kidogo au kutopewa
kwa wakati
ix. Fedha za uhamisho
na likizo; kwa mfano kuna walimu ambao wameanza kazi 2004 NIT Shule ya msingi
Dar es Salaam wamelipwa fedha za likizo mara moja mwaka 2012, mfano halisi ni
mwalimu Ruth Natumwa, huyo ni kati ya walimu hao. Matatizo ya walimu kimsingi
ni janga la taifa, yapo Taifa zima, kwa mfano katika shule ya Sekondari Kizota,
Dodoma kuna walimu wengi wana madai yao dhidi ya Serikali, waliajiriwa
mwaka jana Machi, wakaanza kupata mshahara mwenzi wa tisa…walilipwa mshahara wa
mwezi wa tisa tu na kuendelea, ile mingine wanaendelea kudai.
x.
Mazingira
magumu ya kazi mijini na vijijini (tunapozungumzia mazingira magumu inahusisha
kutokuwepo vitendea kazi au kuwa vichache, miundo mbinu duni nk).
xi. Waajiri
kutochangia mifuko ya jamii
xii. Fedha za makato ya
wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii zimekuwa zikikopeshwa watu wengine wasio
wanachama wakiwamo wanasiasa huku wafanyakazi wenyewe wakiendelea kuwa na
maisha duni
xiii. Kufanya kazi kama kibarua kwa miaka mingi
jambo ambalo ni tofauti za sheria za kazi
xiv. Huduma za kifedha kuwa mbali na maeneo ya
kazi, hali inayosababisha wafanyakazi kutumia fedha nyingi kufuatilia mishahara
kwa vile ni mbali na eneo wanalofanyia kazi.
xv. Kutokuwa na mfumo
unaoeleweka wa upandishaji vyeo na ujira/malipo kwa wafanyakazi/vibarua
xvi. Waajiri hasa binafsi kufukuza wafanyakazi
hovyo/no job security…kufanya kazi bila mikataba
xvii. Kupambana na tatizo la kodi kubwa kwa
mishahara (PAYE)
xviii. Tatizo la mabosi kutoa upendeleo wa wazi kwa baadhi
ya wafanyazi kwa sababu zisizo za kitaalamu; wakati mwingine ni kwa sababu ya
ngono; kuwataka kimapenzi wafanyakazi ili waendelee kuwepo kazini au
kupandishwa vyeo…tatizo hili linaonekana kuwa sugu, wanawake wengi maofisini
hawako huru sana, wamekuwa wakitakwa kimapenzi mno na mabosi wao, wengi
wanashindwa kujizuia, tunataka kuona kunakuwa na sheria kali dhidi ya mabosi wa
aina hii kama ilivyo katika nchi nyingine.
Ndugu
wanahabari
Tatizo
la ajira kuporwa na wageni
Ingawa
sheria/sera za ajira zinaeleza wazi kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini
zaidi ya watano kwa kazi ziziso na ujuzi, baadhi ya makampuni yamekuwa
yakiingiza wageni kwa kazi ambazo Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.
Ndugu
wanahabari Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni
pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni kweli hakuna Watanzania wenye
sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.
Ndugu
wanahabari
Nitapigania
kuhakikisha tabia ya waajiri kulazimisha waajiriwa lazima wawe na uzoefu mkubwa
inapungua au kukoma kabisa
Kigezo cha kupata ajira kiwe ni uwezo wa mtu wakati huo baada ya kufanyiwa
usaili, siyo lazima awe na uzoefu wa miaka mitatu au mitano kama ambavyo
waajiri wengi wanalazimisha; tunahitaji kuona Serikali inasimamia hili. Kama
hali ni hii, wahitimu wanawezaje kupata ajira? Ni suala ambalo nitakuwa mkali
nalo mno kwa sababu lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania, limekuwa ni sababu
ya rushwa ikiwamo ya ngono…walioko vyuoni wengi hawana uhakika wa ajira, kwa
sababu ya tabia hii. Ni lazima tubadilike, watu waajiriwe kulingana na uwezo
wao wa kazi, siyo uzoefu.
Ndugu
wanahabari
Wanafunzi
shule ya Msingi/Sekondari nk wapatiwe elimu ya kujiajiri.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.
Ndugu
wanahabari
Nitaanzisha
idara mbili mpya na kuboresha zilizoko;
i. Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair Foundation www.wheelchairfoundation.org.
i. Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair Foundation www.wheelchairfoundation.org.
Ndugu
wanahabari
Kutakuwa
ni mikakati mbalimbali kuhusu wafanyakazi walemavu na wale wanaopata ulemavu
wakiwa kazini, kwa mfano Mwenyekiti wa Wasioona mkoani Tanga amekuwa ni mtu
ambaye ameumia kazini, lakini aliishia kulipwa Sh150,000 na bandari ambako
alikuwa anafanya kazi kama kibarua. Kitendo kitakuwa na jukumu la
kufuatilia kwa ukaribu hali za wafanyakazi walemavu, kuangalia kama wanavyotoka
vyuoni wanapewa ajira au wanaishia kunyanyapaliwa? Utafiti unaonyesha kuna
wanafunzi wengi wanaohitimu masomo wakiwa na ulemavu, hata hivyo hawaonekani
kwenye maofisi wakifanya kazi. Wanakwenda wapi? Litakuwa ni jukumu la hicho
kitengo.
Ndugu
wanahabari,
Idara ya pili ni
Idara
ya fursa/Career Development Department na Mafunzo
Nimetembea
katika nchi tofauti Duniani ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius,
India, Thailand, Sweden na Marekani…nimeona fursa kadhaa ambazo zimenishawishi kuanzisha
idara maalum ya kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa zinazoendelea Duniani na
hapa nchini. Fursa hizo zitakuwa zinapatikana katika tovuti za TUCTA na ofisi
za vyama vya wafanyakazi mikoani. Baadhi ya fursa ni namna gani mtu anaweza
kusoma nje ya nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi, fursa ya
mashirika ambayo yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali.
-Kwa
mfano kuna mashirika kama www.nuffic.nl au vyuo ambavyo mtu anaweza kusoma
bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu ya Marekani na fursa
nyingine nyingi. Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki sana na fursa hizi.
Ziko pia taasisi nyingine zinatoa.
Ndugu
wanahabari
Idara
hii itakuwa na majukumu ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuzifahamu sheria za
kazi, hali kadhalika itakuwa inawasiliana na waajiri ili zaidi ya barua ya
ajira au mkataba wanaompa mwajiriwa, ampe pia na chapisho letu ambalo
mwajiriwa anapaswa kupewa siku ya kuajiriwa kwake ili ajue kwa uhakika sheria
za kazi zinasemaje; haki ya mwajiriwa kwa mwajiri au ipi na haki ya mwajiri kwa
mwajiriwa ni ipi; tutashawishi hili liwe ni suala la lazima. Tutakuwa na vituo
maalum vya msaada wa kisheria mikoani kote au kwenye kanda. Tutakuwa na vipindi
kwenye televisheni angalau kila mwezi mara kuelezea masuala ya sheria za kazi.
Tutaitumia tovuti ya TUCTA kuwa ya kisasa zaidi.
Ndugu
wanahabari
Kulifufua
gazeti la Mfanyakazi ndani ya siku 90 ili liwe sauti thabiti ya wafanyakazi
Haijalishi
kama TUCTA itakuwa na fedha au la, nitahakikisha ndani ya siku 126
litakuwa mitaani likiandika habari mbalimbali hasa likitumika kama sauti ya
wafanyakazi na yote ambayo yataonekana ni ya maana kwa ustawi wa taifa. Nina
uzoefu zaidi ya miaka 20 katika sekya ya habari kama Mhariri, na hata sasa ni
Mhariri wa Biashara gazeti la Mwananchi, nitahakikisha tunatafuta fedha ndani
na nje ya TUCTA ikiwamo kuwatumia wafanyabiashara kwa kubadilishana msaada kwa
matangazo kwa muda, ili hatimaye liweze kuwa mitaani. Ni aibu kubwa kuona nchi
ina wafanyakazi wengi, lakini gazeti kama hili la wafanyakazi haliko mitaani.
Ndugu
wanahabari
Kuimarisha
uhusiano wa vyama vya ndani na vyama vya nje
Nitahakikisha
nafanya mawasiliano na mashirika mengine yakiwamo International Trade Union
Confederation, Secretary General Sharan Barrow na mashirika mengine ili
kuona namna gani vyama vya wafanyakazi vya nchini vinanufaika na ushirikiano
huo kwa kubadilishana uzoefu na kadhalika mara kwa mara kadri inavyowezekana.
Ndugu
wanahabari
Nitatutumia
uzoefu wangu wa shughuli za kuwasiliana na vyuo vya nje na uzoefu wangu wa
kufanya kazi katika mashirika mbalimbali ya nje kama muwakilishi wao hapa
nchini, na kutembea nchi mbalimbali, kuviunganisha vyama vya ndani vya
wafanyakazi, kuwa na ukaribu zaidi na vile vya nje, na pia kujenga uwezekano wa
viongozi nchini kwenda nje kupitia ushirikiano huo.
Ndugu
wanahabari
Hili
linawezekana kwa njia mbili, kwanza kama washirika wetu kwa vile tutakuwa tuna
mawasiliano ya karibu na aina ya chama ambacho mtu anatoka, kwa mfano kama COTWU,
TTU, TALGWU, TUICO, TAMICO, TEWUTA, DOWUTA, TPAWU, RAAWU, TUGHE, CHODAWU,
TRAWU. Nahitaji kuona ofisi za vyama vya wafanyakazi nchini zinakuwa za kuvutia
kwa kuzipatia vitendea kazi, kuna mashirika nayafahamu, tunaweza kuyatumia
kuwasiliana nayo yakatusaidia kama vile Computer Aid International la Uingereza
ambalo hutoa misaada ya computer za aina mbalimbali kwa nchi maskini kama
Tanzania (www.computeraid.org).
Nje ya hiyo nitakuwa na vikao na viongozi wa chama kimoja badala ya kingine
kuangalia namna gani tunaweza kuboresha shughuli za utendaji za ndani na nje
hasa kuimarisha rasilimali watu na vifaa. Lengo kubwa la kuomba niwe Rais wa
TUCTA ni kuangalia namna gani tunaweza kushirikiana na wafanyakazi na viongozi
wa vyama katika kuimarisha wafanyakazi, kwani malalamiko ni mengi. Tutaendeleza
mali za TUCTA zikiwamo Chuo cha Wafanyakazi Mbeya na maeneo mengine.
Ndugu wanahabari
NAMNA
GANI HAYA YATAWEZEKANA?
Mkakati
wa kuondoa kero zote zilizoelezwa juu utafanikiwa kwa majadiliano yenye ukomo
(deadline) na Serikali/waajiri, au kufanya chochote ambacho katiba inaruhusu.
Sheria ziko wazi, nitahamasisha zifuatwe na zifahamike. Shida kubwa ninayoiona
kwa sasa, wafanyakazi wengi hawajui haki zao pia msaada wa vyama katika
kuwasaidia wafanyakazi ni mdogo.
Ndugu
wanahabari
Hata
hivyo mkakati hasa ni kuangalia TUCTA kwa kushirikiana na vyama shiriki
vinafanya nini kuondoa changamoto ambazo sisi wenyewe tunaweza kuziondoa.
Uongozi siyo kulalamika, bali kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuondoa shida
zilizoko. Tayari nimeanza kuwasiliana na vyama mbalimbali vya wafanyakazi
katika mataifa ya nje ili kuangalia namna gani tunashirikiana kwa maana ya
kubadilishana uzoefu nk.
Ndugu
wanahabari
Ofisi
nyingi za vyama vya wafanyakazi zimechakaa, naangalia uwezekano wa kushirikiana
nao katika hili kwa njia ya kutafuta wafadhili wa nje au kubuni miradi
itakayosaidia kuondoa hali hiyo; nataka pia maisha ya viongozi wa vyama vya
wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla yabadilike kwa kutumia jitihada hizo
nilizozieleza juu, nafahamu vizuri namna ya kusaka wafadhili, kwani ni shughuli
ambayo nimekuwa nikifanya kwa muda mrefu kupitia taasisi yangu ya Global Source
Watch, niliyoianzisha toka mwaka 2001 ambayo imekuwa ikifanya kazi ya
kuwaunganisha watu na vyuo zaidi ya 78 vya nje kama Marekani, Canada, Greece,
India, Malaysia nk.
Ndugu
wanahabari
Nafahamu
kuna vyama vina miradi ya maendeleo, vinawasaidiaje wanachama wao? Nahitaji
niwe Rais ili nishirikiane na vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla
kuleta tija kwa Watanzania. Tusiwe watu wa kunyoosheana vidole…kila mtu awe
chanzo cha mabadiliko anayotaka kuyaona Tanzania! Naamini kila mtu akifanya
kazi zake vizuri…Tanzania itakuwa na maendeleo kwa kasi. Wafanyakazi wanahitaji
mambo mengi zaidi ya kuhamasishwa migomo, lakini kama tutaamua kugoma,
tunapaswa kugoma kwa kumaanisha, hatupaswi kuogopa kutekeleza yaliyo haki yetu.
Ndugu wanahabari
Kwa
nafasi nitakayokuwa nayo nitaanzisha semina, makongamano, mijadara itakayokuwa
ya wazi na kutoa elimu ya kutosha juu ya haki za wafanyakazi na wajibu wa
waajiri kwa wafanyakazi. Hii itasaidia kupunguza migogoro na wafanyakazi
watatambua haki zao.
Ndugu
wanahabari
Tunatakiwa
kuwa sauti ya wafanyakazi hapa Tanzania, TUCTA imelala, tunataka kuikimbiza
mchakamchaka,, kuna mambo mengi yanatokea dhidi ya wafanyakazi hapa nchini
lakini TUCTA haitoi hata matamko au kutetea wafanyakazi,
Ndugu wanahabari
Natambua
changamoto za wafanyakazi, tunataka kuwa na
TUCTA
Mpya
Nguvu
Mpya
Uongozi
Mpya
Sauti
Mpya
Umoja
Mpya
Maendeleo
Mapya
Kwa
pamoja tunaweza.
Mungu
awabariki!
Dismas
Lyassa
Mgombea
nafasi ya Urais-TUCTA simu 0754 49 89 72
HOTUBA
FUPI KUTOKA KWA JEBRA KAMBOLE, Wakili wa Dismas Lyassa anayefanya Kampuni ya
Uwakili ya Law Guards Advocates ya Jijini Dar-es-salaam kwa Waandishi wa
Habari.
Ndugu
waandishi wa Habari wa vyombo vyote vya Habari,
Ndugu
watanzania wengine mliopo hapa,
Shukrani
Tunashukuru
sana kwa kuitikia wito wetu, Mungu awabariki sana, Tunamshukuru mwenyezi mungu
kwa kutupa afya na sia njema,
Ndugu
waandishi wa Habari
Kuna
mambo muhimu manne tunataka kuwaeleza watanzania wote, hasa wafanyakazi na
viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi
Moja,
Ndugu anatimu iliyojipanga makini kuhakikisha TUCTA inarejea na kuwa na Nguvu
zaidi, Ni kijana makini mwenye malengo ya kuleta maendeleo ya haraka na kufufua
uhai wa TUCTA.
Ndugu
Waandishi wa Habari
Napenda
kuchukua fursa hii kutoa onyo kwa wanaopanga kutoa rushwa kwenye huu uchaguzi
wa TUCTA kuwa tuko makini na hili tumejipanga, tutachukua hatua za haraka za
kisheria dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwaripoti kwenye vyombo husika, Rushwa
si kipaumbele utapinga kwa nguvu zetu zote.
Ndugu
Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa pia atasaidia kuanzisha kituo au kushirikiana na mashirika mengine
kutoa masaada wa kisheria kwa wafanyakazi wanaofukuzwa makazini kinyume cha
sheria. Wafanyakazi wengi wakikumbwa na matatizo wafanyakazi wenzao
wanawatenga, vyama vyao vinawatenga, Dismas atahakikisha kuwa TUCTA ni kimbilio
lao.
Ndugu
Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa atasaidia kutoa mafunzo ya kisheria kwa wafanyakazi ili waweze
kutambua haki zao za msingi, kwa kuendesha semina, makongamano na mijadara
itakayotoa elimu na kuibua mijadara kwa wafanyakazi.
CHAGUA
DISMAS LYASA KWA TUCTA MPYA, Mabadiliko ni sasa,,,Asanteni
0 comments:
Post a Comment