Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KAMPUNI YA DRIVE DENTSU YAFUNGUA OFISI ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM

KAMPUNI YA DRIVE DENTSU YAFUNGUA OFISI ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Drive Dantsu, Cheriff Tabet (wa tatu kulia), akiwa na viongozi mbalimba wa kampuni hiyo wakati wa kutambulisha kwa wanahabari kufunguliwa kwa ofisi hiyo nchini Dar es Salaam jana.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Drive Dentsu imepiga hodi kwa kufungua ofisi zake jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada  za kusogeza huduma zake kwa wateja wake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Cherrif Tabet alisema kampuni hiyo iliyotanda nchi takriban 110 ni sehemu ya muunganiko wa kimataifa wenye zaidi ya wafanyakazi 37000 na ofisi 160 duniani kote.

"Ni muungano ambao unaleta pamoja ujuzi, maarifa na vitendea kazi vyenye kuhakikisha inawapa wateja wake huduma zenye ubora wa hali ya juu" alisema Tabet.

Alisema ufunguzi wa ofisi hiyo jijini Dar es Salaam umelenga kutoa suluhisho la ubunifu kwa makampuni na bidhaa za kitanzania.

Tabet alisema pamoja na kuwekeza hapa nchini kampuni hiyo imelenga kujipanua katika masoko mengine katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kuhakikisha wanakidhi mahaitajai yao kwa kutoa sukluhu kwa changamoto zote za kibiashara.

"Katika ukanda wa Afrika Mashariki, uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kasi kubwa pamoja na ongezeko la uzarishaji wa bidhaa nyingi jambo ambalo linakuza mazingira yenye ushindani hivyo kufanya kuwepo na uhitaji mkubwa wa ubunifu katika kuwafikia wateja" alisema Tabet.

Meneja Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Rami El Khalil alaisema Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kutokana na uchumi wake kuwa imara hivyo ni sehemu nzuri kuwekeza.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa