Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAONYESHO
ya bidhaa za Kichina yanatarajiwa kufanyika Agosti 21 hadi 24 mwaka huu
kwa madhumuni ya kuendeleza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China
hususani katika masuala ya biashara.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari jana,mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya viwanda,
biashara na Kilimo, Bw.Daniel Machembe alisema kuwa maonyesho hayo
yanatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Alisema kuwa maonyesho
hayo ni kwa ajili ya kuendeleza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na
China hususani katika masuala ya biashara ambapo sasa yanafanyika kwa
mara ya tatu katika mwaka huu.
Alisema kuwa maonyesho
ya mwaka huu yanatarajia kuhusisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na
mashine,magari, vifaa vya nyumbani,vifaa vya umeme pamoja na vifaa vya
ujenzi.
Mkurugenzi huyo alisema
kuwa kumekuwa na uhusiano mzuri baina ya Tanzania na China tangu mwaka
2001 ambapo Tanzania ilianza kupeleka bidhaa mbalimbali kuuza nchini
humo kwa ajili ya kuingizia pato Taifa.
Alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kupenda bidhaa zenye ubora.
Alisema kuwa China
imepata fursa nzuri kwa ajili ya kufanya maonyesho ya bidhaa zao
Tanzania kwa ajili ya kuendeleza na kukuza uchumi.
Alisema kuwa thamani ya
biashara kati ya China na Tanzania mwaka jana ilifikia dola za
Kimarekani bilioni 3.7 ambayo imezidi kwa asilimia 49 kuliko ilivyokuwa
mwaka 2012 na kuweka rekodi mpya.
"Tunatarajia bidhaa za
mwaka huu zitaendelea kuwa bora kutokana na urafiki wa muda mrefu uliopo
kati ya China na Tanzania, kwani China imekuwa ikifanya maonyesho
nchini kwa ajili ya kukutana na Wafanyabiashara wakubwa na kuwauzia
bidhaa mbalimbali," alisema.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment