CRDB
Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote
ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni
zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya
bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa
Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African
life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia
Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.
CRDB
Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma
hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha
jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na
Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile
‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David
na wengine ni Herry pamoja na Jonas.
Huduma
hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania
wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini
Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya
mikono salama" .
Meneja
wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto)
akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa
kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia)
wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni
jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea
kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance
Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life
Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala
Manyama.
Meneja
Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia)
akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy
Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment