Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WIZARA KUZIBANA KAMPUNI ZISIZOSAJILIWA

WIZARA KUZIBANA KAMPUNI ZISIZOSAJILIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema haitatambua kazi za upimaji zinazofanywa na kampuni zisizosajiliwa, ikiwa ni mkakati kuepuka migogoro ya ardhi.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa wizara hiyo, Justo Lyamuya alisema kazi zote za upimaji viwanja zitakazowasilishwa wizarani, ambazo hazikufuata taratibu na kwa mujibu wa Sheria ya Upimaji Ardhi Sura 324 ya mwaka 1957, hazitapokewa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Lyamuya alisema Serikali iliunda Halmashauri ya Taifa Wapima Ardhi (NCPS) kwa jili ya kusajili wataalamu wapima ardhi na kampuni za upimaji ardhi na wathamini.
Alisema hadi sasa idadi ya wapima ardhi, waliosajiliwa ni 290, kampuni zikiwa 58. Wathamini waliosajiliwa ni 320 na kampuni zilizosajiliwa ni 54.
“Kwa kuwa kuingia na kusaini mikataba ya udanganyifu ni kosa la kisheria, mikataba yote mibovu itapelekwa kwenye vyombo vinavyosimamia sheria, ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa” alisema.
Alisema kampuni za upimaji zinazopitisha na kuwasilisha kazi kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, ambazo hawakuzisimamia wenyewe au wawakilishi wao na kuthibitika, hazitapokewa. Badala yake, zitaadhibiwa ikiwemo kusimamishwa kwa mujibu wa sheria.
Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa