Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizindua Rasmi huduma mbili mpya kutoka mfuko wa Pensheni wa PSPF ambazo ni Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanza Maisha. Katika hotuba yake Mheshimiwa Gaudentia Kabaka aliupongeza mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kuwa wa kwanza kubuni huduma hii ambayo sio tu kuwasaidia wanafunzi lakini pia waajili ambao ndio watakuwa wanaanza maisha kwa kupewa mkopo, Pia aliwapongeza PSPF pamoja na Benki ya Posta Tanzania kwa wote kujiunga pamoja kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kiutendaji kazi. Mh. waziri alihimiza watu kufuata masharti na sheria za mfuko ili waweze kunufaika zaidi. Alimalizia kwa kuutaka Mfuko wa PSPF kuendelea kuwa na ubunifu zaidi ili wanachama wake waendelee kunufaika zaidi na kufaidi Matunda ya Mfuko huo wao na vizazi vijavyo.
Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifungua pazia ishara ya kuzindua Rasmi huduma
mbili mpya kutoka mfuko wa Pensheni wa PSPF ambazo ni Mkopo wa Elimu na
Mkopo wa kuanza Maisha.
Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka wa kwanza kushoto akiwa na Furaha pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bwana Adam Mayingu wa kwanza kulia na Afisa Mtendaji mkuu wa Benki ya Posta Bwana Sabasaba Moshingi mara baada ya uzinduzi huo Rasmi.
Wakinyoosha Mikono Baada ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bwana Adam Mayingu akitoa Hotuba yake wakati wa uzinduzi Rasmi wa Huduma mpya kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , katika Hotuba yake amezungumzia kuwa mkopo wa elimu anaweza akaupata mtu yoyote yule na kwa kiwango cha elimu kuanzia Sta Shahada , kwa upande wa Mkopo wa kuanza Maisha Mkurugenzi Mkuu wa PSPF alisema kuwa ni mkopo ambao utawasaidia wafanyakazi wengi hasa wale ambao ndio kwanza wamepata ajira kwa kuwapa mkopo wa Mshahara wao wa Miezi miwili ili fedha hizo ziwasaidie kuanza kujipanga kimaisha na lengo kubwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anatimiza ndoto zake , Mwisho alisisitiza kwamba huo sio Mwisho wa huduma bali wanachama na wafanyakazi wakae mkao wa kula mambo mazuri mengi yanakuja kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Afisa Mtendaji mkuu wa Benki ya Posta Bwana Sabasaba Moshingi akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi huo ambapo Mfuko wa Pensheni wa PSPF unashirikiana na Benki ya Posta Tanzania kufanya kazi pamoja, Katika salamu zake alielezea ushirikiano wao na PSPF, Pia alizungumzia kwa ufupi juu ya Huduma mpya za PSPF ambapo na wao wanashirikiana kwa pamoja
Muwezeshaji wa Sherehe hiyo ya Kuzindua Huduma Mbilia za PSPF Bwana Njaidi Akiendelea Kutoa Mwongozo
Balozi wa PSPF Mwanamuziki Mkongwe na Mwenye nyimbo za kipekee zenye mahadhi ya Aina yake Vibwagizo na Vionjo vyake vitamu Mrisho mpoto akielezea na kufafanua pia kuwaelimisha wageni waliofika katika Hafla hiyo ya uzinduzi wa Huduma mpya Mbili za PSPF kwa kuwaeleza nini maana ya PSPF ilitokea wapi, Alielezea Mafao yatolewayo na Mfuko wa PSPF katika mpango wa lazima ambayo ni Fao la Uzeeni,Fao la ulemavu, Masharti ya Mirathi, Fao la Kufukuzwa/ Kuachishwa kazi, Fao la Kujitoa na fao la Uzazi, lakini hakuishia hapo alielezea pia Mafao yatolewayo katika Mpango wa hiari ambapo alisema ni Fao la Elimu, Fao la Ujasiliamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/ Ulemavu na Fao la Kujitoa na Mwisho alielezea Mikopo itolewayo na PSPF ambapo alisema ni pamoja na Mkopo wa Elimu, Jipange Maisha:Mkopo kwa waajiriwa wapya , Mkopo wa Nyumba , Mkopo wa wastaafu wenye Masharti nafuu.
Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF Bwana Masha akitoa neno la Shukurani baada ya kumalizika kwa Sherehe hizo
Meza Kuu wakisikiliza kwa makini kinacho endelea katika uzinduzi huo
Baadhi ya Watumishi na Wageni waaalikwa wakiwa wanafuatilia Jambo kwa makini
Balozi wa PSPF Mrisho Mpoto akifurahia Jambo
Wageni waalikwa , watumishin wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika sherehe hiyo
Picha ya Pamoja
Picha na Dar es salaam yetu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Picha na Dar es salaam yetu
Leo Desemba 11, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa
kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa wateja wake,
huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.
Kwa upande
wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu
katika ngazi yoyote ile ya elimu, mfano stashahada, shahada, shahada ya uzamili
na hata mafunzo ya ufundi. Katika huduma
hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 4.
Kwa upande
wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa
ana mahitaji muhimu, kwa kutambua hilo PSPF imeanzisha mpango huu ambapo mwanachama
anaweza kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili aweze kujipanga na maisha
mapya ya ajira. Katika huduma hii PSPF
imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.
Lengo kubwa
la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake
ikiwa ni katika masomo kwa kupitia mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa
kupitia mkopo wa kuanzia maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania wenzetu kujiunga na PSPF ili waweze kufaidika
na fursa hizi.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudentia kabaka
alisema amefurahishwa na PSPF jinsi ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania
katika Kubuni, Kupanga, kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema hili
ni jambo sahihi na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii duniani kote, kazi za Mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha
wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanastaafu.
Kwa upande
wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi alisema
mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la
Benki ya Posta lililopo karibu yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni za
haraka sana na bora.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
1 comments:
naomba kuuliza,kama mwajiriwa mpya na mwanachama mpya katika mfuko wa PSPF,naweza kupata/kuomba mkopo baada ya muda gani?
Post a Comment