Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee
wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari katika makao
makuu ya mfuko huo wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo
ulitunukiwa nchini Morocco na Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi
wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi
Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na
Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa katika mkutano huo uliozungumzia
tuzo hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee
wa pili pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo kulia Mkurugenzi
wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi
Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na
Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko
huo kutoka Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA)
nchini Morocco hivi karibuni
Kwa miaka
mingi sasa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa mwanachama wa
mashirikisho mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirikisho la kimataifa la
Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA), Shirikisho la Hifadhi ya Jamii la
Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), na Shirikisho la kimataifa la
Uchumi wa Afya (IHEA). Mashirikisho haya husaidia katika kubadilishana
uzoefu katika maeneo mbalimbali, ushauri wa kitaalamu, viwango vya
huduma, miongozo ya kiutendaji pamoja na kutumika kama jukwaa kwa
wanachama kujenga na kuhamasisha mifumo endelevu katika hifadhi ya
jamii. Taasisi hizi za kimataifa vilevile huhusika katika kutoa tuzo kwa
Taasisi ambazo zinafanya vizuri katika ubunifu katika maeneo
mbalimbali.
Shirikisho
la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) limekuwa na
utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye
maswala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo;
kuboresha huduma, utawala bora, matumizi ya teknolojia, ukusanyaji wa
michango na matekelezo, uwekezaji, kufikisha huduma kwa wananchi waliyo
sehemu ngumu kufikika, uhamasishaji wa Afya na uepushaji wa hatari
makazini, pamoja na utekelezaji wa tathmini za uhai wa mifuko.
Mashindano haya yalianza tangu mwaka 2008 na hufanyika kila baada ya
miaka mitatu.
Tangu
kuanzishwa kwa tuzo hizi, Mfuko umekuwa ukishinda tuzo katika maeneo
mbalimbali. Mwaka 2008 Mfuko ulishinda tuzo moja ya ubunifu katika
kuboresha huduma na mawasiliano kwa wanachama kupitia siku ya wadau
(Clients Days).
Mwaka 2011 Mfuko ulishinda tuzo nne katika masuala yafuatayo;
Uboreshaji wa kitita cha mafao yanayotolewa na Mfuko;
Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii: katika kupanua wigo na jitihada za kufikia lengo la afya kwa Watanzania wote;
Utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na Uboreshaji wa majengo inayotolewa na Mfuko;
Ugatuzi
wa shughuli za Mfuko kwa kufungua ofisi za mikoa kuwasogezea huduma
wananchi: Usimamizi bunifu kuongeza ufanisi katika utendaji.
Kwa
mara nyingine Mfuko umeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya
hifadhi ya Jamii Barani Afrika katika sherehe za kukabidhi tuzo hizo
zilizofanyika tarehe 3 Disemba 2014 katika hoteli ya Sheraton mjini
Casablanca, Morocco. Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la
utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufikika, kazi
ambayo Mfuko umekuwa ukifanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali
za rufaa nchini tangu mwaka 2012.
Tuzo
nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji pamoja na
uwasilishaji wa madai ulioanzishwa kwa dhumuni la kupunguza malalamiko
ya baadhi ya vituo vya Afya kuchelewa kulipwa madai yao. Kupitia mfumo
huu, muda wa ulipaji wa madai hasa katika hospitali kubwa nchini
umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Mfumo huu ulianza tangu Januari 2012.
Tuzo
ya tatu ni juu ya huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu ambayo
imeanza tangu mwaka 2011. Fao la wastaafu linalenga kuwapa wananchi
ambao walikuwa wanachama wa Mfuko na wenza wao uwezo wa kutibiwa kupitia
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kustaafu ajira mpaka mwisho wa
maisha
Mfuko
utaendelea kufuata miongozo inayotolewa na mashirika ya kimataifa ili
kutekeleza shughuli zake kiufanisi na kuhakikisha unatoa huduma bora kwa
wanachama wake.
Mfuko
vilevile unadhamiria kuendelea kuboresha shughuli zake ili uweze
kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la viwango la
kimataifa (ISO) na hatimaye kuthibitishwa kwa kutimiza viwango hivyo
katika kipindi kifupi kijacho.
NHIF
Mfuko pia unatarajia kwa kipindi kijacho kuweza kukidhi viwango
vilivyowekwa na Shirikisho la kimataifa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
(ISSA) na kupata ithibati ya kukidhi viwango vya kimataifa.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment