Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto)
akimwapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof.
Musa Juma Assad, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad
akisaini hati ya kiapo chake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto)
akisaini hati ya kiapo cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za
Serikali Prof. Musa Juma Assad mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania
Mohamed Chande Othman wakati wa hafla fupi ya kuapishwa kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini
Dar es salaam, Kulia ni Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mh. Zitto
Kabwe akisalimiana na Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya wakati wa hafla
fupi ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za
Serikali Prof. Musa Juma Assad(wa pili kutoka kushoto) na wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali leo Ikulu jijini Dar es
salaam.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda
akizungumza jambo la baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali mara baada ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya
wa Hesabu za Serikali Ikulu jijini Dar es salaam.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano uliopo kati ya
Ofisi yake kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika
kujenga Mfumo wa kisasa wa ukaguzi wenye uwajibikaji unaojenga nidhamu
katika mapato na matumizi ya Serikali.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad
akiongea na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyotekeleza majukumu
yote yaliyoainishwa katika ofisi yake kwa mujibu wa sheria.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad
(aliyeshika maua) akipongezwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya
kuapishwa leo. Kulia ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali
aliyestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria Bw. Ludovick
Utouh.(Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment