Home » » WADAU WAJITOKEZA KWA WINGI TAYARI KUSHIRIKI MAONESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA ELIMU, DAR‏

WADAU WAJITOKEZA KWA WINGI TAYARI KUSHIRIKI MAONESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA ELIMU, DAR‏

Na Mwandishi Wetu.
Wadau wa Elimu ndani na nje ya nchi wamejiandikisha kwa wingi tayari kwa kushiriki maonesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu nchini ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, pamoja na kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje Global Education link.
Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa ya aina yake kuwahi kutokea nchini yanawashiriki kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi,Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi,Asasi za kielimu za ndani na nje ya nchi ambazo huto udhamini kwa wanafunzi.
Katika maonesho hayo kutakuwa na banda maalum la Watanzania wataalam wanaosoma nje ya nchi katika fani za sayansi na teknolojia hasa masomo ya gesi na mafuta ambao watatumia fusra hiyo kutoa ushauri na elimu zaidi namna nchi zilizoendelea zinavyotumia fusra hizo pamoja na kuwashauri vijana wakitanzania ilikuweza kupata elimu sahihi hasa kwenye masuala mtambuka kama gesi na mafuta ambazo zimegunduliwa nchini Tanzania.
Mratibu wa maonesho hayo mkurugenzi mtendaji wa Global Education Link ,Abdulmalik Mollel (Pichani) amesema hii itakuwa fusra ya kipekee wa vyuo vya elimu ya juu hapa nchini kutoa maelezo ya kina kwa kozi pamoja huduma wanazotoa ilikujenga uelewa sahihi kwa wazazi,wanafunzi wa sasa pamoja na wanafunzi ambao wanatarajiwa kujiunga vyuo vikuu hivi karibuni.
Tume ya vyuo vikuu TCU watakuwa sehemu ya wadau muhimu wa elimu ambao watatumia maonesho hayo kutoa maelezo kwa wanafunzi waliohitimu ngazi mbalimbali ambao wanatarajia kujiunga vyuo vikuu hasa namna ya kufuata taratibu za kuomba udahili kwa umakini bila kukiuka taratibu.
Maonesho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’ Yatashirikisha wadau wanaotoa huduma za elimu kama vile wanaouza vifaa vya elimu sare za shule na vyuo,vifaa kama vile thamani , kemikali za mabara,makampuni na mashirika yanayotoa zabuni za vyakula pamoja na mifuko ya hifadhi za jamii.
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
MOENESHO HAYO YATAANZA TASMI TAREHE 17 HADI 21 DESEMBA KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE MAARUFU KAMA SABASABA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa