Home » » LIMBU ASIMAMISHWA UENYEKITI ACT

LIMBU ASIMAMISHWA UENYEKITI ACT

CHAMA cha ACT-Tanzania kimemsimamisha aliyekuwa Mwenyekiti wake wa muda, Kadawi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya ndani ya chama hicho.
Akitangaza maazimio ya Chama hicho, yaliyotokana na Mkutano wa Halmashauri Kuu Taifa uliofanyika juzi, Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya wajumbe 57 kati ya 65 sawa na asilimia 87.7 waliohudhuria mkutano huo kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa viongozi hao.
Alisema katika mkutano huo wa pili wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya ACT Tanzania pamoja na mambo mengine, ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali na kutoa maamuzi na maazimio, yakiwemo yanayowahusu viongozi hao.
Mwigamba alisema kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho, adhabu hiyo itakuwa ya miezi sita bila kuwasimamisha nafasi za uanachama wao huku wakiruhusiwa kugombea katika nafasi mbalimbali katika mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaotarajiwa kufanyika Machi 28 Mwaka huu.
Alitaja baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na kuitisha kikao haramu kinyume cha Katiba na kuwafukuza wenzao uanachama, kusababisha mtafaruku ndani ya chama kutokana na vikao hivyo pamoja na kukiuka taratibu zingine.
Chanzo: Habari Leo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa