Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe.
Hayo yalibainishwa jana na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe, wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kikao chake katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, jana.
“Kamati inampongeza huyu TR mpya maana anaonyesha kuwa na uwezo mzuri wa kufanya kazi……..ataweza kuokoa mapatp mengi ya serikali,” alisema kabwe.
Kabwe pia aliongeza kuwa, kamati hiyo imemwagiza TR huyo kumteua mkaguzi anayejitegemea kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa hesabu za taasisi hiyo ya fedha ambayo serikali ina hisa.
Kwa mujibu wa Kabwe, kamati hiyo jana ilikuwa inapitia taarifa kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Shirika la Pride kwamba liliondolewa kimakosa katika orodha ya mashirika ya serikali na kesho kutwa inatarajia kupata taarifa kamili kuhusu shirika hilo na hasara ambayo serikali imepata.
Pia ilikuwa inapitia taarifa za Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) kuhusu utendaji wake, mitaji na matatizo mengi yakiwamo ya gawiwo lake ‘divident’ la asilimia 25 kutoka kampuni ya simu ya Airtel na hivyo kutakiwa kujadiliwa tena Januari 21 mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment