Suleiman Kova, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
.
Kati yao vijana 163 toka katika manispaa za Temeke na Kinondoni wamefanyiwa uchunguzi, na muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Vijana hao waliokamatwa ni pamoja na wapiga debe katika vituo vya daladala, wacheza kamari, wavuta bangi, watumiaji wa dawa za kulevya na watumiaji wa pombe haramu ya gongo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema tangu Januari 5 hadi 7, mwaka huu wamekamatwa Panya road 240 na kati yao, 95 uchunguzi wao umekamilika na watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
“Operesheni hii ni endelevu, lengo ni kufuta kabisa jina la Panya road pamoja na kuondoa makundi yote ya wazururaji, wavuta bangi, dawa za kulevya pamoja na watumiaji wa pombe haramu ya gongo,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya, alisema juzi waliwakamata vijana 57 ambapo ma kufikisha jumla ya waliokamatwa 225 na kati yao 68 uchunguzi dhidi yao umekamilika na watapelekwa mahakami muda wowote.
Baada ya kundi hilo kutikisa Jiji la Dar es Salaam,Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilianzisha kamatakamata na operesheni Jiji zima kwa lengo la kukabiliana na makundi hayo ya kihalifu hasa kundi hilo.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment