WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake
pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi
katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Wakiongozwa na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili,
wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza
kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.
Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali, Mwana FA akitumia
tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana
kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua
viongozi wanaowataka.
“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni
sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala
nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele
na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.
Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa
sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani
hapo.
Mbali na Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani
hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi
sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na
Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and Kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge,
Temba, Mwasiti, Godzilla na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya
mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro
ambapo lina lengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na
kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao
utafanyika Oktoba mwaka huu.
PICHANI JUU: Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza
katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya
MwembeYanga jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa
OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa
wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya
sabasaba jana jioni mjini Morogoro.
Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk'
akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January
lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
Baadhi ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi
lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo
jana.
Wasanii Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika
tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga
Mkali mwingine wa kughani mitindo huru, Godzilla akitumbuiza jana
jioni katika viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar,kwenye tamasha la
Tuo8January, lililofanyika hapo jana.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa
morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo
jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa
morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo
jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Wasanii Aika, na Nahreel wanaounda kundi la Navy & Kenzo
wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja
vya MwembeYanga, Temeke jijini Dar.
Baadhi ya wadau wakirekodi tukio muhimu
Pichani Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka mbele ya
mashabiki wake huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala
uwanjani hapo jana.
Wasanii Madee na Dogo Janja ( hayupo pichani) wakitumbuiza katika
tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya
MwembeYanga,Temeke jijini Dar.
Hii ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza
kuunga mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha
vijana kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi. Picha kwa
hisani ya Mdimuz Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment