Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr JAKAYA KIKWETE amekua na utaratibu wa mara kwa mara wa
kuwatembelea na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa hospitali.
Safari hii Rais
KIKWETE amewatembelea na kuwapa pole wagonjwa kadhaa waliolazwa katika
hospitali ya Taifa Mhimbili na Hospitali kuu ya Jeshi LUGALO jijini Dar es
salaam
akiwemo Brigedia Jenerali Mstaafu HASHIM MBITA, Meja Jenerali Mstaafu Maneno,
Brigedia Jenerali Mstaafu FAKI na Kanali S.A Fallah
Rais KIKWETE pia ametumia nafasi hii kuona
upanuzi wa majengo muhimu unaoendelea katika Hospitali kuu ya Jeshi LUGALO kwa
lengo kuboresha huduma za hospitali hii muhimu
0 comments:
Post a Comment