Wajumbe kutoka Wizara
na Taasisi mbalimbali jana walikutana katika ofisi za Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuzungumzia maazimio yaliyofikiwa kutoka
katika kikao cha kwanza kilichowakutanisha wasambazaji wa filamu wakiwasilisha
malalamiko yao kwa mheshimiwa waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.
Wajumbe hao kutoka
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Wizara ya Viwanda na
Biashara,Wizara ya fedha,Shirika la Mapato Tanzania(TRA),Shirika la Viwango
Tanzania(TBS) na Tume ya Ushindani
walizungumzia kwa mapana maazimio hayo kumi tatu(13) kama kutoa ushauri kwa
kampuni mbalimbali za simu kuchangia maendeleo ya wasanii wanaowatumia,Shirika
la Mapato Tanzania pia liongeze udhibiti katika filamu za nje zinazoingizwa
nchini na filamu hizo zifuate sheria,kanuni na Taratibu kabla ya kuingizwa
sokoni na kukazia swala la hakimiliki iongezwe nguvu ili iweze kupambana na
suala la uharamia.
Akitoa hoja katika
majadiliano hayo Katibu mtendaji wa Bodi
ya filamu Bi.Joyce Fissoo alishauri Shirika la Mapato Tanzania kuendelea kutoza
kodi filamu za nje kwani zitalinda viwango vya filamu izi na pia udhibiti
uongezeke katika uingizaji wa filamu za nje.
Nae Afisa Mtendaji
Mkuu kutoka COSOTA Bi. Doreen Sinare aliwasihi wasanii kuwa
makini na kuuza hakimiliki za kazi zao na kukazia kwamba chama cha hakimiliki
kipo kwa ajili yao kwaiyo wasisite kuwatembelea kwa ajili ya ushauri wa
kisheria na pia kusajiri kazi zao cosota.
Kwa upande wake
mjumbe kutoka Tume ya ushindani Bi.Martha Kisombe alisisitiza kuwa chombo chao kipo kwa ajili ya kulinda na kukuza
ushindani katika soko na kumlinda mlaji kutokana na masuala yote yasiyo na
usawa na upotoshaji wa kimauzo.
Aidha ,Afisa Viwango
kutoka Shirika la Viwango nchini Bw.Henry Massawe alieleza upande wao
wataendelea kusimamia viwango katika soko la Filamu ili kupata kitu bora pamoja
na kusimamia CD/DVD zinazotoka nje ziwe na kiwango kizuri.
Kikao hicho cha
wajumbe kilikutana pia na wasambazaji wa filamu ili kuwapa mrejesho wa maazimio
waliyofikia katika kikao cha kwanza ambapo kikao hicho kilihairishwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilly Beleku kutokana na wasambazaji
hao kuja na zaidi ya watu walioalikwa katika kikao hicho na hata alipowaomba
kutoka wale wasiohusika walipinga.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao ili kujadili suala la bei za filamu wakiwa wanamskiliza Kaimu mkurugenzi wa Utamaduni(hayupo pichani),Bi.Lilly Beleku walipokuwa wakijadili swala zima la bei za filamu wakizungumzia haswa kuzingatiwa kwa bei kutokuwa chini sana kuliko gharama za uzalishaji.
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka COSOTA,Bi Doreen Sinare akielezea jinsi wanavyowasaidia wasanii kwa kuwapa ushauri unaofaa katika kazi zao na swala zima la uharamia katika tasnia nzima ya filamu.
Wajumbe kutoka bodi ya filamu wakimskiliza kwa makini Dkt. Mona Mwakalinga(aliyevaa Miwani) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Idara ya sanaa na maigizo walipokuwa wakizungumzia swala zima la ukuaji wa filamu nchini na Bei zake kwa ujumla.
Wajumbe waliohudhuria kikao cha
majadiliano ya maadhimio yanayohusu bei za filamu wakiskiliza kwa makini
maadhimio yaliyofikiwa katika kikao cha kwanza.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.





0 comments:
Post a Comment