Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji
Mketo amesema chama cha wananchi CUF kimepanga kulipeleka jina la
mwenyekiti wa CUF taifa Profesa Ibrahimu Lipumba katika umoja wa katiba
ya wananchi-UKAWA- ili kuomba ridhaa ya kugombea kiti cha urais dhidi ya
majina yatakayoletwa na wagombea wa vyama vingine vinavyounda umoja
huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu tarehe za kuchukua fomu
kwa wagombea wa udiwani, ubunge na kiti cha urais, Bwana Mketo amesema
kwa mujibu wa makubaliano na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi kila chama kitateua mgombea katika nafasi zote na kisha
kushindanisha ili kupata mgombea moja atakayeungwa mkono na vyama vyote.
Aidha amesema katika nafasi ya viti vya udiwani na ubunge kwa
wanaotaka kugombea fomu zitaanza kutolewa kuanzia machi 1 hadi 10
kupitia makatibu wa matawi na katika nafasi ya ubunge wagombea
watatakiwa kuchukua fomu kwa makatibu kata na kuzirudisha kwa makatibu
wa wilaya ambapo amesema aprili 17 hadi 19 kurugenzi ya uchaguzi
inatarajia kukaa na kufanya mchujo kwa wagombea ubunge
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment