Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAMA AJERUHI MTOTO WAKE WA MIAKA MIWILI

MAMA AJERUHI MTOTO WAKE WA MIAKA MIWILI

Mtoto Christina Kusale (2) amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kufanyiwa ukatili na mama yake mzazi kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Amesema Ofisa Ustawi wa Jamii wa hospitali hiyo, Dk Rose Temu kuwa mtoto huyo ambaye anaishi Kinondoni alipelekwa na majirani baada ya kusikia akipigwa na mama yake.
Temu alisema waliingia ndani na kumkuta mtoto huyo akilia huku akiwa na majeraha yanayodhaniwa ya kisu na kumsababishia maumivu hayo.
“Mtoto Christina alifikishwa hospitalini hapa Februari 22, mwaka huu akiwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili wake ambayo yalikuwa sehemu za usoni, mikononi, kwenye makalio, mapaja na mgongoni,” alisema Temu.
Alisema amelazwa wodi namba mbili akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Alisema mama wa mtoto huyo anashikiliwa na Polisi na uongozi wa hospitali unafanya utaratibu ili aende kwa ajili ya kuchunguzwa kama ana matatizo ya akili.
Wakati huohuo, mtoto anayekisiwa kuwa na umri wa miezi minane ametelekezwa katika eneo la Mbezi na kuokotwa na msamaria mwema aliyempeleka katika Kituo kidogo cha Polisi Mbezi.
Alisema mtoto huyo alipelekwa katika hospitali hiyo juzi saa 9 alasiri na alifanyiwa uchunguzi wa vipimo mbalimbali na hawakubaini tatizo lolote.
“Tunategemea kesho (leo) kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto Msimbazi,” alisema Temu.
Matukio ya ukatili kwa watoto yanaendelea kuripotiwa baada ya jamii kupata elimu ya kutosha kuhusu tatizo hilo na haya ni matunda ya wadau wanaotoa elimu kila kukicha.
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa