Na. Aron Msigwa –
MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2015 umepungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia
4.8 ya mwezi Desemba, 2014 kutokana na kuendelea kupungua kwa kasi ya bei ya
bidhaa na huduma mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa ya
mfumuko huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa mfumuko wa
Bei katika maeneo mbalimbali nchini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei
ya bidhaa za vyakula na zile zisizo.
Amesema kiwango cha
badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya
kimeonyesha kupungua katika maeneo mbalimbali nchini kikihusisha bei ya
mahindi, Unga wa mahindi , ndizi, ndizi za kupika na mihogo.
Aidha, Bw. Kwesigabo
ameeleza kuwa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa
bei nchini ni pamoja na mafuta ya taa asilimia 8.4, dizeli asilimia 10.2,
Petroli kwa asilimia 6.8 na gesi ya kupikia
kwa asilimia 2.9.
Akitoa ufafanuzi kuhusu
kiwango cha badiliko la kasi ya bei za
bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi kwa kipimo cha mwezi kati ya
mwezi Desemba 2014 na Januari 2015 , amesema kuwa mwezi Januari umekuwa na ongezeko
la asilimia 1.0 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 2.0 la mwezi Desemba ,
2014.
Kuhusu Fahirisi za bei
kwa maana ya kiwango cha badiliko la kasi ya bei za makundi ya bidhaa na huduma zote
zinazotumiwa na Kaya binafsi kwa kuzingatia kipimo cha mwezi zimeonyesha kuongezeka
hadi kufikia 152.43 kwa mwezi Januari 2015 kutoka 150.92 za mwezi Desemba,
2014.
Amebainisha kuwa
kuongezeka kwa Fahirisi hizo kumechangiwa na bidhaa za mchele, nyama, samaki
,lishe kwa watoto, mbogamboga, mavazi ya wanawake, kodi ya pango na mkaa kwa
asilimia 1.6 .
Kwa upande wa uwezo wa
shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi
Januari , 2015 Kwesigabo amesema kuwa umefikia shilingi 65 na senti 60
ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 66 na senti 26 za mwezi Desemba 2014.
“Uwezo wa shilingi 100
ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi
Januari 2015 na Desemba 2014 umepungua kidogo, hii inamaanisha sasa mtu hahitaji
kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa na huduma anazozihitaji”
Kwa upande wa mfumuko
wa Bei wa mwezi Novemba 2014 katika nchi za Afrika Mashariki amesema una
mwelekeo unaofanana , Kenya ukipungua na
kufikia asilimia 5.53 kwa mwezi Januari
2015, kutoka asilimia 6.02 za mwezi Desemba 2014, Uganda mfumuko wa bei kwa mwezi Januari 2015 umepungua
hadi asilimia 1.3 kutoka asilimia 1.8 za mwezi Desemba 2014.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment