Rais Mstaafu wa
awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akiongozana na jaji mkuu wa
Tanzania, Mohamed Othaman Chande (watatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadiki (wa kwanza kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,
na Jaji
Kiongozi wa
Mahakama Kuu, Shabani Ally LILA wakiwa katika matembezi ya
kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam February 1, 2015.
Bendi ya polisi ikiongoza
matembezi ya wiki ya sheria nchini.
Watumishi wa Mahakama nchini
pamoja na watumishi wa taasisi zingine wakiwa wakiwa katika matembezi ya
kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam February 1, 2015.
Matembezi yakiwasili katika
uwanja wa mnazi mmoja.
Vijana kutoka katika vikundi
mbali mbali wakitoa burudani wakati wa kuadhimisha wiki ya sheria nchini.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto),akipata maelezo
kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw.
Michael Mhando kuhusiana huduma wanazotoa NHF alipokuwa akitembelea mabanda ya
maonesho ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini (kushoto katikati), jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande, na
kulia Meneja Masoko na Elimu kwa Umma NHF, Bi. Anjela Mziray.
Wtumishi wa Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),wakiendelea kutoa elimu kwa washiriki wa
maonesho hayo namna ya kujiunga na NHIF (wakwanza kulia), Afisa
Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi. Catherine Kameka, na katikati Afisa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF, Bi Hawa
Duguza.
Washiriki
wa maonesho hayo wakipata huduma mbalimbali kutoka kwenye banda la NHIF.
Rais Mstaafu wa
awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Naibu Msajili wa Mahakama ya
Rufaa, Bi. Zahra Maruma juu ya huduma zinazotolewa alipotembelea banda hilo (wa
kwanza kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadiki.
jaji
mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande akizungumza kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuzindua wiki ya
sheria nchini yanayofanyika katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu
wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake wakati akizindua wiki ya
sheria nchini katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu
wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Majaji waliokaa mbele wakiwa
kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika wiki
ya sheria nchini.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Ali
Hassan Mwinyi ameitaka jamii
kuacha kuchukua sheria mkononi na badala
yake waviache vyombo vya dola vifanye kazi yao
kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni jambo
la dhuluma na aibu.
Aliyasema hayo February 1, 2014 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fursa ya kupata haki: wajibu wa serikali,mahakama na wadau."
Alisema kuwa katiba Ibara ya 107 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanuia inae lekezakuwa mahakama ndio muhimili pekee uliopewa jukumu na dhamana ya kuwafikishia haki.
"ili Mahakama kutekeleza majukumu hayo lazima wananchi wajengewe uelewa juu ya shughuli za mahakama zinavyoendeshwa na hilo ndio lengo la maadhimisho haya,"Alisema Mwinyi Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajijengea utaratibu wa kuisadia mahakama pindi panapo hitajika ushahidi ili kuepuka kuachiliwa huru kwa wahalifu wao kwa kukosa ushahidi wa kutosha.
Alisema kuwa sheria pia inahitaji Majaji na Mahakimu watoe haki kwa kuzingatia sheria hivyo ni wajibu wa wananchi na jamii nzima kushirikiana na mahakama kupata haki halali kwa watuhumiwa wetu.Kwaupande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman alisema kuwa mahakama imedhamiria kutoa elimu kwa ummma kuhusu masuala mbalimbali ya kimahakama.
Alisema kuwa wamejipanga katika kutoa elimu kuhusu ufunguaji na uendeshaji wa mashauri mbalimbali,utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu muafaka pamoja na mfumo mpya wa kulipa tozo za mahakama kwa njia ya benki. "kwa mara ya kwanza mahakama ya tanzania imeamua kushirikisha jamii katika kujifunza jinjsi utendaji kazi wa mahakama unavyofanya kazi ni matumaini yetu kuwa jamii itajifunza vyema na kutii sheria za nchi"alisema Chande.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment