Na. Aron Msigwa
Dar es salaam.
SERIKALI
imetoa wito kwa watafiti na wataalam kutoka vyuo vikuu, taasisi za elimu na
mashirika binafsi kushiriki kikamilifu kuhamasisha jamii kutumia takwimu
sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kuwezesha upangaji
wa mipango endelevu ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya maeneo husika.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati akifungua
warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka
Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya Elimu ya
Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na Wadau wa mbalimbali wa
maendeleo, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Hajjat
Amina Mrisho Said amesema kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya
takwimu sahihi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Amesema
wadau hao pamoja na mambo mengine wanalo jukumu la kuielimisha jamii
kuelewa mchango wa takwimu katika kufanikisha masuala mbalimbali ya taifa
pamoja na uandaaji wa sera za maendeleo.
Bi.
Hajjat amesema Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekuwa ikifanya
mabadiliko makubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa takwimu zinazokusanywa
kutoka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji
nchini.
“Tanzania
sasa inafanya maboresho na mabadiliko makubwa ya takwimu zake sasa tunazo
takwimu mbalimbali na mkakati wa kuzisambaza takwimu hizo kwa watumiaji
ili waweze kuzifanyia kazi unaendelea” Amesema .
Akizungumza
kuhusu umuhimu warsha hiyo amesema inalenga kuwaweka pamoja wazalishaji na
watumiaji wa takwimu kutoka katika maeneo mbalimbali ili waweze kujadili
changamoto mbalimbali, kubadilishana uzoefu na kupeana mrejesho wa matumizi ya
takwimu zilizopo hapa nchini.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe
akizungumzia umuhimu wa warsha hiyo kwa washiriki hao amesema kuwa
imewakutanisha wadau hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na kupima mafanikio ya
shughuli za kitakwimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Ameongeza
kuwa warsha hiyo ya siku 2 inalenga kuwawezesha wadau hao kuangalia changamoto
mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu katika
maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia mahitaji
yanayojitokeza pande kwa wazalishaji na watumiaji.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment