Katibu mkuu ofisi ya waziri
mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI ) Jumanne Sagini amesema
hatasita kuchukua hatua stahiki, ikiwemo kuwafukuza kazi baadhi ya wakurugenzi
wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji watakaobainika kushindwa kusimamia
matumizi ya fedha za umma na miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo.
Ametoa onyo hilo wakati
akifunga mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma yaliyowashirikisha wajumbe
wa bodi za ununuzi, wanasheria na wakurugenzi wa halmashauri nane zinazotekeleza
mradi wa uimarishaji wa miji 18 ya tanzania bara, yaliyofadhiliwa na benki ya
Dunia kwa ushirikiano na taasisi ya kiufundi ya ubelgiji kwa lengo la
kuzijengea uwezo halmashauri hizo katika kuandaa na kusimamia mifumo ya ununuzi
kwa weledi na tija zaidi.
Katibu mkuu huyo ameongeza
kuwa manunuzi yanatumia zaidi ya asilimia 70 hadi 80 ya bajeti za halmashauri,
hivyo amewasisisitiza watendaji hao kuhakikisha wanasimamia kwa weledi wa
kutosha katika eneo la manunuzi ili kuondoa malalamiko na kasoro mbalimbali
ambazo zimekuwa zikibainishwa katika taarifa ya kila mwaka ya mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.
Aidha Sagini amedai kuwa
kumekuwepo na tatizo la utumiaji wa fedha pasipo kufuata taratibu sahihi,
ucheleweshaji wa maamuzi ya kufanya manunuzi kwa wakati kutokana na wataalam
kutokuwa na uwezo wa kutosha katika ununuzi, utayarishaji wa nyaraka sahihi za
ununuzi na uamuzi wa aina ya njia ya ununuzi, mambo ambayo amesema yanachangia
katika utekelezaji mzuri wa kandarasi husika.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma
kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment