Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, 05/02/2015
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 22
wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu
Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG)
utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa na Mahasibu Mkuu wa
Serikali Mwanaidi Mtanda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile jana jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika nchini.
Mhasibu Mkuu wa Serikali Mwanaidi
alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Katika mkutano huo, mada mbalimbali zinatarajiwa
kujadiliwa zikilenga kwa lengo la kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi
wanachama katika masuala ya hesabu za serikali na kutoa fursa ya kuwa na jukwaa
kwa ajili ya washiriki ili kufanya tathmini kwa kujadiliana na kushirikishana
uzoefu mbali mbali.
Aidha, mkutano huo unalenga kuhamasisha
maendeleo ya watendaji wahasibu wa Serikali na kutoa mafunzo stahiki kupitia
utekelezaji wa program shirikishi kwa kujifunza uzoefu wa masuala mbali mbali
ndani ya nchi wanachama.
Mkutano wa wahasibu hao unatarajiwa kuwa
na washiriki zaidi ya 1000 wakiwemo Wahasibu wakuu 14 kutoka nchi wanachama na
wadau wengine.
Ujio wa wageni hao pamoja na ushiriki
wao katika mkutano wa siku tano utakuwa wa tija na fursa muhimu katika utoaji
wa huduma za jamii wakati wote watakapokuwa nchini.
Aidha, katika mahitaji yao ya malazi,
chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi, makadirio ni kwamba kila mgeni
anaweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja, hivyo basi kwa hesabu za haraka
haraka kutakuwa na matumizi ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano
katika muda wa siku tano tu.
“Wito wangu kwa watanzania, nawaomba
wajitokeze kushiriki katika mkutano huu wa ESAAG wa 2015, hivyo natoa rai kwa
wataalam, wahasibu na wadau wetu wote kwa ujumla wao ili tuweze kushirikiana
kuufanikisha mkutano huu wa kimataifa unaofanyika nyumbani, Tanzania” alisema Mwanaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi
Kifile amesema kuwa nchi washiriki zinazounda umoja huo ni Botswana, Kenya,
Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini,
Swaziland, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
Azizi aliwahakikishia washiriki wote
kuwa maandalizi ya mkutano huo katika masuala ya usafiri, usalama na malazi
yapo katika hatua nzuri na kamati yake imejipanga vema ili mkutano huo uwe wa
mfano wa kuigwa kwa nchi zote wanachama watakapopata fursa ya kuandaa mkutano
wa mwaka katika nchi zao.
ni wa serikali wa nchi za mashariki na
kusini mwa Afrika,Kwa bahati nzuri chama hiki kikiwa na malengo yafuatayo
ESAAG ni chama cha wahasibu wakuu ambacho
kilizaliwa miaka 20 iliypoita Arusha hapa nchini mwaka 1995 na mkutano wa mwaka
huu wa 22 wa ESAAG unaongozwa na kauli mbiu “Uimarishaji na usimamizi wa fedha
kwa ajili ya Maendeleo ya kijamii na Kiuchumi katika kanda’’.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment