Home » » MH. DKT KABWE STEVEN KABWE NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AKABIDHI BWENI LA WAVULANA NA NYUMBA YA MAMA MLEZI, MAKAO MAKUU YA TAIFA YA WATOTO KURASINI.

MH. DKT KABWE STEVEN KABWE NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AKABIDHI BWENI LA WAVULANA NA NYUMBA YA MAMA MLEZI, MAKAO MAKUU YA TAIFA YA WATOTO KURASINI.

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kabwe Steven Kabwe (wa Pili kulia) Akikata Utepe ishara ya Kukabidhi rasmi Bweni la Wavulana na Nyumba ya mama Mlezi Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini . Kushoto ni Beatrice Mgumilo Mama Mlezi wa Kituo na katikati ni Makamu wa Rais wa Abbot Fund Tanzania Andy Wilson.
Mgeni Raami  naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kabwe Steven Kabwe akiongea na wageni pamoja na watoto wanaoishi Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini. Katika hotuba yake Mh. Naibu Waziri aliushukuru Mfuko wa Abbot Tanzania kwa kutoa fedha zao za Ufadhili na kukarabati bweni la wavulana na nyumba ya mama mlezi katika makao ya Taifa ya watoto Kurasini.

Pia Mh. Dkt Kwabwe alitoa shukurani zake kwa ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mfuko wa Abbot Tanzania katika kuwezesha utekerezaji wa Mipango mbalimbali hapa Nchini. "Nafahamu kwamba ushirikiano huu ulianza tangu mwaka 2000 kupitia mfuko wa Abbott Laboratories kwa wakati huo ambao ulikuwa unalenga katika kupunguza makali ya Maisha kutokana na UKIMWI na Virusi vya UKIMWI pamoja na huduma kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi nchini." aliongea Dkt. Kabwe

Aliongeza kuwa kupitia ushirikano huo makao ya Taifa ya Watoto Kurasini yalikuwa ni kati ya Miradi aliyofadhiriwa na Mfuko huo, ambapo alisema shughuli zilizofanyika katika makao haya ni pamoja na Kufanya ukarabati wa majengo wa majengo yaliyokuwepo ambayo ni mabweni ya watoto,zahanati,jiko,bwalo la chakula,vyoo uwanja wa kuchezea watoto, Kuimarisha huduma ya chakula na lishe kwa chakula na lishe kwa watoto,kuwapatia watoto huduma za afya na matibabu, kuwapatia watoto mahitaji na vifaa vya elimu na kuwapatia watoto/vijana Mafunzo ya Tehama.

Mwisho Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Kabwe alimalizia kwa kutoa maagizo kwa wahusika wa Makao ya Taifa ya watoto Kurasini kuhakikisha wanakarabati majengo hayo kwa kila miaka mitatu na kuzingatia usafi na afya Bora kwa watoto, Na kusisitiza kuwa watoto wanapokuwa wakubwa ni vizuri wakahamishwa na kwenda maeneo ya vituo vya kulelea watu wazima.

 
 Watoto wakimsikiliza kwa Makini Mgeni Rasmi
 Naibu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Rabikira O. Mushi akizungumza jambo wakati wa Sherehe hiyo
 Makamu wa Rais wa Abbot Fund Tanzania Andy Wilson akizungumza na wageni waalikwa pamoja na watoto wa kituo hicho cha Taifa, ambapo alisema kuwa Abbott wameendelea kufadhili na kusapoti mambo mbalimbali katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi mbalimbali kama ya kuku, kusapoti katika upatikanaji wa maji, afya bora kwa watoto katika kituo hicho, kilimo kupitia bustani ndogo ndogo, kuwakuza kielimu hasa ya Tehama na Umeme. Pia aliishukuru Serikali ya Tanzania na wafadhiri kama Abbott katika kuendelea kutoa misaada kwa wahitaji.
Mama Mlezi wa Makao Makuu ya Taifa ya Watoto Kurasini akitoa Shukurani zake kwa ujenzi wa Jengo la kisasa kwa ajili ya Kuishi Mama Mlezi na Bweni la Wavulana na kuomba kuwa watu wengine zaidi wajitokeze kwa ajili ya Kusaidia kwa kuwa kunachangamoto nyingi ikiwemo Ada za watoto kwenda Shule, Nauli na mambo mengine, alishukuru Shirika la Abbott Tanzania kwa kuendelea Kusapoti  kituo hicho.
Watoto wakiimba wimbo maalum wa Shukurani kwa mgeni Rasmi pamoja na Wageni waalikwa
 Nuru Dotto Dada Mkuu wa Kituo hicho akizungumza jambo wakati wa Sherehe hizo za kukabidhiwa Bweni la wavulana na nyumba ya mama Mlezi
 Gungu Benedicto  Kaka Mkuu wa Kituo hicho akizungumza jambo wakati wa Sherehe hizo za kukabidhiwa Bweni la wavulana na nyumba ya mama Mlezi
 Mgeni Raami  naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kabwe Steven Kabwe  akikagua Jengo hilo
 Moja ya Mabweni hayo.
Jengo hilo ambalo lilizinduliwa

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa