JUMLA
dola za Kimarekani Milioni 31 (zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania)
zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo
la Tabata Relini, Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando
wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari,
Tabata, Dar es Salaam.
Mhando
mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo
Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na
Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora
kuliko nyingine zote nchini.
“Ni
studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni kubwa
kama CNN, Aljazeera BBC, na kwa kuwa za kwetu ni mpya, zinaweza kuwa na
ubora kuliko hizo,”amesema.
Tido
amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo, zoezi la uzinduzi
wake rasmi litafanyika kesho, asubuhi mjini Dar es Salaam.
Mhando
ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu enzi zake nchini
kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), alisema mgeni rasmi katika
uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Mrisho Kikwete.
“Azam
TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini
tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho, ambayo
tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam TV,”alisema Tido.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment