Katika
Kanisa la Living Water Centre Kawe siku ya jana kulikuwa na mahafali ya
11th ya kozi inayoitwa Life Transforming kozi ambayo inakuwa ni darasa
la kukulia maisha ya wokovu au darasa la utumishi katika Ufalme wa
Mungu.
Apostle
Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Kawe
ambaye ndio kiongozi wa kozi hiyo alikuwepo kuhudhuria mahafali hayo,
ambayo kozi hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi wachache ambapo
kadri miaka inavyokwenda idadi imekuwa ikiongezeka, na tangu chuo kianze
mwaka huu ni mahafali ya 11.
Mahafari
hayo yalipambwa na Uimbaji,Maigizo,dance na shuhuda za kile ambacho
Mungu amewatendea wanafunzi hao katika kipindi chote walichosoma.Wengi
wao katika shuhuda wamesema darasa hilo limewafundisha kumtumikia Mungu
zaidi
Wakitoa
shukrani zao kwa Mungu na mtumishi wamesema kuwa wamefundishika vyema
kwa sababu wapo tofauti sana na walivyokuwa awali kabla ya kuanza darasa
na wamefanyika utu upya na kwao hadi jana wanahitimu darasa wamepata
mabadiliko makubwa.
Katika
risala yao walisema kuwa elimu hii ya kozi ya Life Transformation
imewapa msingi na kutujenga kiroho na kimwili, pia imewapa uwezo wa
kujitambua na kufikiri, kufanya mambo kwa usahihi na kufanya maamuzi
thabiti juu ya maisha yao,kwa msaada wa Roho mtakatifu, aliye msaidizi
wetu. Imetuwezesha kufahamu kiundani maana ya wokovu na umuhimu wa
wokovu katika maisha yetu. Tumepata elimu sahihi juu ya jinsi ya
kuukulia wokovu, kuwa waadilifu, kuwa na moyo wa msamaha, kujua nafasi
ya kiongozi wa kiroho, nini hasa maana ya imani na utakatifu kwa ujumla
wake. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kulisoma neno na kujua msaada mkubwa
uliopo katika neno kwenye maisha yetu na jinsi itupasavyo kuliishi
neon, Alisema msoma risala.
Katika
kozi hiyo wamekuwa wakisoma na kufanya majaribio ya mitihani mara kwa
mara jambo lililowasaidia kuwainua katika kukua kiroho na pia wakaahidi
kuyaishi yale mema yote waliyo yapata katika darasa hilo ili kuzidi
kufikia lile kusudi la Mungu aliloliweka juu yao.
Kozi
hiyo huwa inafanyika katika kanisa la Living Water Centre Ministry
Makuti Kawe Dar es Salaam kila mwanzoni mwa mwaka mwezi January kwa
miezi 3-4.Tangu miaka kadhaa imepita hadi mahafali hii ya mwaka 2015
kozi hiyo imesaidia watu wengi kuwa watumishi wazuri wa Mungu kutokana
na masomo wanayojifunza
Baadhi ya wanafunzi walihitimu Life Transformation koziwakitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada |
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry na Mke wake Lilian Ndegi wakifuatilia shuhuda kwa umakini sana |
Mhitimu akitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada |
Baadhi ya wahitimu wa darasa hilo wakitoa shukrani zao kwa waalimu na watumishi waliohusika kuwafundisha. |
Wahitimu wa darasa hilo wakiimba katika kwaya yao ya pamoja |
Furaha kiongozi wa kwaya hiyo akiongoza nyimbo. |
Umati wa waumini na ndugu wa wahitimu walipohudhulia ibada hiyo kuja kuwatazama ndugu zao |
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment