Mjasiriamali
na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David
Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo
aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda
vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
Mmoja
wa wajasiliamali ambaye pia ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu
wake wa jinsi alivyo nufaika na mafunzo kama haya na mpaka sasa
anajitegemea na Kupata kipatochake na kuwasaidia wengine.
Wa
kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada ambaye amekuwa mfano mzuri
wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi wake umuhimu wa mikutano
kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna
Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata
elimu Bora ya Kilimo.
Bwana Daniel Ambaye ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake katika maswala ya kilimo.
Mwendeshaji
msaidizi wa Semina Hiyo Bwana Saidi akitoa mafunzo ya juu ya kuanzisha
kilimo kwa kutumia Green House pamoja na faida zake
Wanasemina
wakiwa wanasikiliza kwa makina mada mbalimbali ambazo zilikuwa
zikitolewa katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa
Semina ikiwa inaendelea
Baadhi ya wanasemina wakiwa katika Picha ya pamoja
Kilimo
na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa
kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji
wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata
mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji
Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary
David Kinong'o.
Katika
Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo
cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu
ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza
kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha
Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.
Pia
walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi
ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za
kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi,
Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji
asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na
badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.
Mwisho
Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza
kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama
wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.
Tembelea Libeneke lake la: www.kukuprojecttz.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment