Home » » DC ILALA, ORIJINO KOMEDI WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KATA YA KIVUKONI‏

DC ILALA, ORIJINO KOMEDI WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KATA YA KIVUKONI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.

Wadau mbalimbali kutoka Green WastePro Ltd, Manispaa ya Ilala, Forum CC pamoja na wasanii mbalimbali wakiendelea kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi kata ya Kivukoni katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Hali ilivyokuwa kabla ya kufanya usafi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shay o(kulia) wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Kushoto ni Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi, Lukac Mhavile "Joti"
Wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiendelea zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akizungumza jambo na Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda wakati wa zoezi la kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi eno la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo ( wa tatu kutoka kulia) akifaya usafi na wadau mbalimbali kwenye wiki ya Mazingira eneo la Agha Khan jijini Dar, wa pili kutoka kulia ni Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena.
Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya Hindi.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) ili kuzungumza na wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira, wa kwanza kulia ni Afisa Usafishaji Manispaa ya Ilala, Bw. Charles Wambura.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa