PROGRAMU
mpya za utamaduni na ubunifu zinatoa fursa kubwa ya uanzishaji wa
shughuli za kitamaduni zenye kuimarisha sekta ya ubunifu wenye mwelekeo
kiuchumi.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
Kwa
mujibu wa balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe, amesema kwamba
Tanzania inautajiri mkubwa wa kiutamaduni ambao unaweza kutumiwa kuchangia pato
la taifa GDP.
“Bado tasnia ya sanaa
na ubunifu ambayo ingeliweza kuchangia katika uchumi na kuwapatia kazi vijana
haijatumika ipasavyo. Kutokana na hilo kipaumbele cha programu hii mpya ni
kuwezesha vijana kutumia sanaa na ubunifu kukuza ajira,” anasema balozi Johnny
Flentoe.
Mshairi Jasper Sabuni akifanya kazi ya 'spoken words' wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
Juni 5, 2015, Ubalozi wa
Denmark ukishirikiana na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU) umezindua
program mpya ya utamaduni na maendeleo Tanzania ( Tanzania Culture and
Development Programme ).
Programu hiyo imelenga
kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo
watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni
na kujipatia kipato.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi wa program mpya ya CKU Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
CKU
inatekeleza program hiyo kupitia kwa washirika wake likwemo Tamasha la
Kimataifa la Filamu (Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kupitia mradi wao
wa Village Panorama ambao unalenga kuonyesha filamu za kuelimisha maeneo ya vijijini
huko Zanzibar.
Taasisi nyingine ni Culture
and Development in East Africa (CDEA), ambao watafanya utafiti wa namba sanaa
ya muziki na filamu inavyochangia katika pato la taifa, wakati taasisi ya Soma
Book Café ikiindesha mashindano ya uandishi na usomaji wa vitabu.
Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wao watanufaika na program hiyo kwa kupatiwa vifaa
vya muziki vya kufundishia huku Nafasi Art Space ambacho ni kituo cha sanaa
kikiboreshwa na kupata uwezo wa kutumika kama kituo kikubwa cha sanaa za
maonesho.
Meneja wa CKU Afrika Mashariki, Christoph Lodemann akitoa maelezo mafupi juu ya program mpya ya Tanzania
“Sanaa ina uwezo mkubwa wa
kuwezesha majadiliano na kupaza sauti ya umma. Ndio maana Denmark inawezesha
kuwapo kwa jukwaa ili wananchi waweze kujieleza wenyewe kupitia sanaa. Kwa
kukuza vipaji vya wasanii wapya nchini Tanzania, Denmark inatoa mchango wake
mkubwa kwa wasanii na wabunifu,” anasema meneja wa CKU Afrika Mashariki Christoph
Lodemann.
Denmark
inawezesha shughuli za sanaa,utamaduni na ubunifu wa kisanii nchini
Tanzania kama mchango wake katika juhudi za kukuza uchumi wa taifa hili.
0 comments:
Post a Comment