Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Danny Paul Njau, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
Mshindi
wa mchezo wa kubahatisha wa Jay Millions, Danny Paul Njau (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya
Simu ya Vodacom kushindwa kumpa zawadi yake ya sh.milioni 100 baada ya
kushinda mchezo huo.
Mshindi
wa mchezo wa kubahatisha wa Jay Millions, Danny Paul Njau (kulia),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya
Simu ya Vodacom kushindwa kumpa zawadi yake ya sh.milioni 100 baada ya
kushinda mchezo huo. Kushoto ni mtoto wake, Erick Danny Njau.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MSHINDI
wa mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions Danny Paul Njau
kupitia jina la Innocent Daniel Njau ametishia kwenda Mahakama
kuishitaki kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushindwa kumpa zawadi yake ya
ushindi sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo wa kubahatisha wa
Vodacom Jay Millions.
Njau ametoa siku saba kwa kampuni hiyo kuhakikisha inampatia fedha hizo vinginevyo atakwenda mahakama kutafuta haki yake.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Njau alisema
amesikitishwa na danadana anazopigwa na kampuni hiyo kushindwa kumpatia
kitita chake hicho baada ya kushinda.
"Tayari
nimetoa malalamiko yangu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha kuhusu suala hilo lakini mpaka hivi sasa bado hajafanikiwa"
alisema Njau.
Njau
alisema kwamba tangu kampuni hiyo ianze kucheza mchezo huo alikuwa
akishiriki kucheza kila siku na ilipofika Januari 14, 2015 saa 5:8
asubuhi kupitia simu yake alipokea ujumbe sms iliyosomeka hivi 'hongera
wewe ni mshindi wa leo wa Tzs Miliioni 100 utapigiwa simu na wafanyakazi
wa Vodacom. Kwa maelezo zaidi ndani ya masaa 48 ambapo alisubiri bila
ya kupigiwa simu kama alivyoelekezwa.
Alisema
Januari 20, 2015 alienda ofisi za vodacom na kuwaelezea kuhusu jambo
hilo ambapo aliambiwa awape muda na aliporudi Januari 22 alikutanishwa
na maofisa wa Jay Millions na kufanyanao kikao akiwepo mwakilishi kutoka
bodi ya michezo ya kubahatisha ambapo aliambiwa kuwa eti sms hiyo ni ya
kwao lakini ilitoka mapema kwenda kwake.
Njau
alisema kwamba kauli hiyo ilimshangaza sana ukizingatia kuwa katika
kipindi hicho cha mchezo kulikuwa na matangazo yaliyokuwa yakisema kila
siku kutakuwa na mshindi mmoja wa sh.100, washindi 10 milioni 10 na
washindi 100 wa sh.milioni 1 na kuwa yeye alifuata taratibu zote za
kucheza mchezo huo Jay kwenda 15544 na kuona sms ya ushindi.
Alisema
baada ya majadiliano na maofisa hao walimuuliza wampe sh. ngapi kwa
kuwa zawadi hiyo imetoka mapema na kabla ya watu hawacheza na kuwa wao
hawana pesa nyingi anayoifikiria.
Alisema
hakuamini kilichokuwa kikifanywa na kampuni hiyo katika uchezeshaji wa
mchezo huo na kuwa aliomba apewe muda wa kutafakari ambapo aliamua
kupeleka malalamiko yake kwenye bodi ya michezo ya kubahatisha na kwenye
vyombo vya habari.
Jitihada
za mtandao huu kumpata mmoja wa maofisa wa Vodacom Tanzania ambaye
alitajwa kuwa ni Meneja, Kelvin Twisa ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo
zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kupigwa zaidi ya mara nne
bila ya kupokelewa, pia hali kama hiyo ilitokea kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas Tarimba ambaye simu yake
ilikuwa imefungwa jitihada hizo zinaendelea ilikutoa fursa kwa maofisa
hao kutoa ufafanuzi ili umma wa watanzania upate kujua kinachoendelea
katika kampuni hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
0 comments:
Post a Comment