Home » » MAJANGILI WAUNDIWA KIKOSICHA MBWA, INTELIJENSIA.

MAJANGILI WAUNDIWA KIKOSICHA MBWA, INTELIJENSIA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu.

Wizara ya Maliasi na Utalii imewasilisha bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 inayoonyesha mikakati mbalimbali ya kukabiriana na tatizo la ujangili kwa kununua silaha na vifaa vya kisasa ili kuimarisha ulinzi wa wanyamapori.
 
Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu (pichani), alisema serikali imejipanga kukabiriana na ujangili na itaanzisha dawati Maalum la intelijensia na kikosi cha mbwa wa kunusa na kufuatilia mienendo ya majangili.
 
Alisema katika mwaka wa fedha uliopita wa 2014/2015 katika hatua za hifadhi na usimamizi wa wanyapori zilijumuisha kuendesha siku za doria 103,895 ndani na nje ya mapori ya akiba.
 
Nyalandu alisema katika doria hizo, watuhumiwa 1,082 walikamatwa na jumla ya kesi 988 zilifunguliwa katika mahakama na kesi 424 zenye watuhumiwa 259 zilimalizika kwa wahalifu kutozwa faini Sh. 258,250,000 na wengine 18 kufungwa jela miezi 26.
 
Alisema nyaraka za serikali zilizokamatwa ni nyamapori yenye kilogramu 9,658 na meno ya tembo 182 yenye uzito wa kilo 256, kucha za Simba 451, meno ya Simba 65, ngozi 60 za wanyamapori mbalimbali, ndege hai 65,kenge 149 na lita 10 za mafuta ya simba.
 
Aliongeza kuwa katika suala la ulinzi wa maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori, Wizara ilipokea taarifa za kuuawa watu 42 katika Wilaya ya Kilwa, Tabora, Tunduru na Ilemela.
 
Nyalandu alisema kutokana na vifo hivyo, serikali ililipa Sh. 36,300,000 kama kifuta machozi kwa ajili ya wananchi 45 waliopoteza maisha na waliojeruhiwa katika wilaya za Singida, Loliondo, Masasi, Serengeti, Tarime, Mpanda,Tabora, Tunduru na Ilemela.
 
Naye Mbunge wa Mbarali (CCM), Dickison Kilufi, alisema kuna mafisadi ambao wanaiandama sekta ya Utalii ambao wanamaliza wanyamapori, lakini hawachukuliwi hatua kutokana na rushwa iliyotamalaki.
 
Kilufi alisema Waziri Nyalandu hivi sasa anaandamwa na mafisadi baada ya kuzuia ulaji fedha ambao unafanywa na baadhi ya watendaji ndani yasekta ya Utalii.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa