Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Marehemu Francis Festus Mengele, enzi za uhai wake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele.
Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa
na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa
mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.
Watoto wa marehemu na dada zake wakiwa kwenye ibada ya maziko makaburi ya Kinondoni.
Ibada ya maziko ikiendelea.
Hali ilivyokuwa wakati wa mazishi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele
likishushwa kaburini.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele
likishushwa kaburini.
Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mazishi hayo.
Ni huzuni tupu.
DC Makonda akiwa udongo kwenye kaburi la Francis Mengele wakati wa mazishi.
Kaburi likijengwe baada ya kuwekwa mwili wa marehemu kaburini.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele.
Waombolezaji wakiwasili makaburi ya Kinondoni tayari
kwa mazishi.
Hali ilivyokuwa makaburini.
Hali ilivyokuwa makaburini.
Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye maziko hayo.
Na Dotto Mwaibale
WASANII mbalimbali wa filamu na bongo fleva wamejitokeza kwa wingi
katika mazishi ya baba ya msanii mwenzao Steve Mengele 'Steve Nyerere,
aliyofanyika juzi makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msanii Jacob Stephen JB ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi ya
marehemu Francis Mengele baba yake na msanii huyo aliyefariki wiki
iliyopita kutokana na maradhi ya mapafu.
Wasanii wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Micky, Vicent
Kigosi 'Ray' Elizabeth Michael 'Lulu' Chuchu Hans, Kajala Masanja
'Kajala' , Mtunzi na muongozaji wa filamu Myovela Mswaisa na wengine
wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyeongoza mazishi hayo
alisema kifo cha Mengele ni pigo kubwa katika wilaya hiyo ya Kinondoni
na familia kwa ujumla.
"Mengele alikuwa na mchango mkubwa katika wilaya yetu ya Kinondoni
katika kulipa kodi kutokana na biashara zake alizokuwa akizifanya na
wingi huu wa watu waliojitokeza katika mazishi yake inaonesha jinsi
alivyokuwa akishirikiana na wenzake hasa waumini wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Usharika wa Kimara alikokuwa akisali" alisema Makonda.
Makonda alitumia fursa hiyo kuiomba Manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi
mitatu kuhakikisha inajenga choo katika makaburi hayo ya Kinondoni
kwani ni aibu kwa eneo hilo kukosa choo hivyo kuwafanya wananchi
wanaofika kwa ajili ya maziko kukosa huduma ya choo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-0712-727062)
0 comments:
Post a Comment