Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Dotto Mwaibale
WAPENZI wa soka
nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 20
mwaka 2015 moja wa moja kwenye luninga zao kupitia ving’amuzi vya StarTimes
pekee.
Michuano hiyo
ambayo itaanza kutimua vumbi tarehe 30 mwezi Mei na kumalizika tarehe
20 mwezi Juni mwaka huu moja kwa moja kutoka nchini New
Zealand ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani
yatachuana kuwania ubingwa.
Akizungumza baada
ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo maarufu
duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa, Makamu wa Rais wa
StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wanafuraha kubwa kuonyesha
michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa zaidi duniani.
“Tunayofuraha
kubwa kuwatangazia wateja wetu kuwa tumepata haki miliki kutoka FIFA za
kuonyesha michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 20 mwaka
2015 itakayofanyika nchini New Zealand. Soka ni mchezo unaopendwa zaidi nchini
Tanzania na barani Afrika kwa ujumla na tunaamini tutawapatia wateja wetu
burudani ya matangazo yenye ubora wa hali ya juu kupitia ving’amuzi vya
StarTimes.” Alisema Bi. Hanif
“Itakuwa ni mara
ya kwanza kwa nchi ya New Zealand kuwa wenyeji wa michuano hii ambayo inalenga
kuyakusanya mataifa pamoja na kukuza umoja na amani. Wapenzi wa soka wataweza
kujionea mechi 52 kutoka kwa timu 24 tofauti. Mchezo wa kwanza utapigwa tarehe
30 Mei ambapo utamkutanisha mwenyeji New Zealand na Ukraine, mechi
itakayoonyeshwa moja kwa moja katika chaneli ya StarTimes Sports 2 inayopatikana
katika ving’amuzi vyote vya dishi na antenna.” Aliongezea
“Ninachoweza
kusema mwaka huu kwetu StarTimes ni wa bahati kubwa sana kwani tumeweza kufanya
maboresho makubwa katika vipindi vyetu hususani vya michezo. Mbali na michuano
hii pia kuna mingine mingi inakuja kwenye king’amuzi hiki hivyo wapendwa wateja
wetu wakae mkao wa kula,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo nawaomba
wateja wetu walipie na wale wasiojiunga wafanye hivyo sasa ili wasipitwe na
uhondo huu.”
Katika michuano
hiyo bara la Afrika linawakilishwa na timu za vijana wa chini ya miaka ishirini
kutoka nchi za Senegali, Mali, Ghana na Nigeria. Huku barani ulaya ni Ureno,
Ujerumani, Austria, Ukraine, Hungary na Serbia; kwa bara la Amerika ni
Marekani, Mexico, Honduras, Panama, Colombia, Brazil, Ajentina na Urugwai; bara
la Asia ni Qatar, Myanmar, Uzibekistani na Korea ya Kaskazini; na pia visiwa
vya Fiji na New Zealand ambao ni wenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
0 comments:
Post a Comment