Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.
DUNIA endelevu haiwezi kuwapo kama hakutakuwepo na bahari yenye kuendeleza uhai.
Miezi michache kabla ya kufanyika kwa kongamano la kihistoria la COP21 (21st Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on Climate Change) la kutengeneza ajenda mpya ya maendeleo endelevu, ujumbe huu ulikuwa hauna tija.
Lakini sasa ujumbe huu una tija sana na muhimu sana.
Iwe nchi iko mbali na bahari au karibu, kila nchi na kila aina ya uhai hutegemea zaidi namna bahari inavyokuwa salama na yenye kutekeleza wajibu wake wa kulea uhai.
Kiukweli bahari ni kitu muhimu katika mfumo wa hali ya hewa duniani, ikiratibu kwa namna ya kipekee mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya hewa na mfupi na pia uwepo wa hewa mbalimbali katika anga ikiwemo oksijeni tunayovuta.
Aidha inawezesha kuwapo kwa lishe na kuwa chanzo cha chakula.
Wakati wanasayansi wanaweka teknolojia mpya kuweza kuangalia tabia za bahari , tunatambua kwamba zipo athari za shughuli za kibinadamu katika afya ya bahari hasa hewa ya ukaa inayozalishwa kwa sababu za shughuli za kiviwanda.
Alisema hewa hiyo ya ukaa imevuruga mfumo wa ikolojia wa baharini na kuweka kazi ya uratibu ya bahari katika hatari.
Kupanda kwa kina cha bahari, kuyeyuka kwa mabonge ya mabarafu, kuzidi kwa kiwango cha tindikali, kuwepo na maeneo yaliyokufa, kuzaliwa kwa mimea bahari hatari, kufumuliwa kwa matumbawe,kupungua kwa samaki na mfumo wa ikolojia… kunaonesha uwapo wa matatizo katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Ili kuangalia athari za shughuli za kibinadamu Unesco inaangalia elimu, utamaduni, sayansi na mawasiliano katika kubadilisha elimu na teknolojia kwa jamii katika maendeeo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi.
Kupitia kamisheni ya bahari dunia, Unesco inaangalia mfumo wa aina yake wa bahari kwa ajili ya utafiti wa hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi.
Pia inawawezesha wataalamu mbalimbali kuchambua matokeo ya tafiti za sasa na hasa kuzidi kwa joto katika bahari na tindikali kwa kutambua thamani bahari katika mabadiliko ya tabia nchi.
Katika Siku ya Bahari , UNESCO kwa kusaidiwa na Monaco, Sweden na Ufaransa, inawezesha tukio kubwa katika makao yake makuu mjini Paris, Ufaransa kuangalia umuhimu wa bahari kabla ya mkutano wa majadiliano wa mabadiliko ya tabia nchi.
Mabadiliko ya tabia na hali ya hewa yana mahusiano makubwa na mabadiliko baharini na hakuna nchi yoyote duniani hata iwe na nguvu kiasi gani cha uchumi inaweza kukabili mabadiliko yanayotokea baharini.
Katika siku hii ya kuadhimisha Siku ya Bahari, ninatoa wito kwa nchi zote wanachama,taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi kushirikiana katika kuhakikisha kwamba dunia inachukua hatua kuona umuhimu wa bahari katika mfumo wa wa hali ya hewa duniani.
0 comments:
Post a Comment