Home » » DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA RIPOTI YA BARABARA MBOVU, AMPA MKURUGENZI WAKE SIKU 14

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA RIPOTI YA BARABARA MBOVU, AMPA MKURUGENZI WAKE SIKU 14

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Julius Mamilo (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda, ripoti ya ukaguzi huo Dar es Salaam leo asubuhi. Ukaguzi huo ulifanyika katika kipindi cha miezi miwili kwa kuwahusisha wataalamu wa masuala ya ujenzi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Paul Makonda (kushoto), akizungumza na wanahabari baada ya kupokea ripoti hiyo. 
Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Julius Mamilo (ushoto), akitoa ripoti hiyo kwa wanahabari mbele ya DC Makonda.


Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amempa siku 14 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kumpelekea taarifa kuhusu ujenzi wa barabara mpya ambazo zimeharibika kutokana na kujengwa chini ya kiwango. 

Makonda ametoa maagizo hayo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipokea taarifa ya ukaguzi wa kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya Kinondoni iliyotolewa mbele yake na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi, Mhandisi Julius Mamilo.

 Makonda alisema kwa muda wa miezi miwili aliunda kamati iliyofanya uchunguzi wa kuharibika kwa barabara hizo na kubaini makosa.

Makonda alisema sababu ya kuharibika kwa barabara hizo ni kutokana michoro yake kutokuwa sahihi na sheria ya wazabuni kutofuatwa, huku usimamizi wa mikataba haioneshi kama miradi ilisimamiwa ipaswavyo.

"Hata suala la kuthamini uwezo wa  wataalamu wa wakandarasi halikuwepo, pia mkataba wa kazi waliofanya na malipo waliopata, hakuna nyaraka ya kuthibitisha hayo," alisema.

Alisema katika kufanikisha mchakato wa uchunguzi wa barabara zilizoharibika, waligundua barabara ya Polisi Mabatini, Akachube ziliharibika kwa kiasi kikubwa, huku zikiwa na muda mfupi tangu zitengenezwe.

"Utengenezaji wa barabara hizo ulibainika kutumia kipindi kifupi mfano ya Akachube na Journalism zilizojengwa kwa siku 120, ikiwa muda huo ni mdogo, kwani ilitakiwa angalau watumie siku 365," alisema.


Alisema ubora wa unene kwa barabara ya Polisi Mabatini haukukidhi viwango, huku kokoto zilizotumika ni ndogo kulingana na zile zinazohitajika na kusababisha kuwa nyembamba tofauti na ilivyotakiwa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu o712-727062)

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa