Home » » MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM APIGA MARUFUKU MAANDAMANO KATIKA KIPINDI CHA KAMPENI.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM APIGA MARUFUKU MAANDAMANO KATIKA KIPINDI CHA KAMPENI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Jiji la Dar es Salaam limepiga marufu maandamno yeyote ya vyama vya siasa hasa wakati wa kampeni na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa chama au wafuasi wowote watakaobainika kufanya maandamo hayo.
Agizo hilo kali kwa wafuasi na vyama vya siasa imekuja siku moja tu kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu, ambapo kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam vyama vyote vya siasa na wafuasi wao watakaofanya kampeni zao Dar es Salaam hawanabudi kuachana na dhana ya maandamo kuelekea kwenye viwanja vya mikutano kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wa jeshi la polisi wanasema wako imara katika kutekeleza agizo hilo na kwamba hawatovumilia chama au kikundi chochote kitakacho sababisha uvunjaji wa amani katika kipindi cha kampeni.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka watendaji katika mitaa kutokukubali watu watakaokufa kwa kipindupindu kuzikwa na ndugu zao kwani inaweza kuwa chanzo cha kuzidi kusambaza ugonjwa huo.


Kwa mujibu wa maafisa wa afya wanasema ugonjwa huu wa kipindupindu wakati wa kiangaza husambaa haraka zaidi, huku ulaji vyakula vilivyopoa, kutokunawa mikono vizuri, ulaji hovyo wa matunda  vikitajwa kuwa moja ya sababu za ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mpaka sasa kunawagonjwa 36 wa kipindupindu huku wagonjwa wapya wakiwa 9 ambapo kata zilizo athirika zaidi zikiwa ni Mwananyamala,  Manzese, Saranga, Kimara, Ubungo,Kigogo, Tandale  na Kijitonyamalas.

Chanzo: ITV Tanzania

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa