Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati, Joseph Mhonda
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, kuhusu amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika
kesho nchini kote. Kulia ni Ofisa Habari wa Makampuni hayo, Pipino
Sudi.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara Habari Maelezo, Vicent Tiganya (kushoto), akizungumza
katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa Habari wa Makampuni hayo, Pipino
Sudi na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati, Joseph Mhonda.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati, Joseph Mhonda
amewataka wananchi kupiga kura kwa amani ili kulinda amani iliyopo
nchini hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini
kote kesho kutwa.
Akizungumza
Dar es Salaam leo Mkurugenzi huyo alisema amani ya nchi inapaswa
kuzingatiwa katika kipindi hiki cha siku ya kupiga kura , siku ya
kutangazwa washindi na siku ya kusubiria majibu ya mshindi.
"Siku
hizi tatu ni ngumu sana lakini ni vyema wananchi wakawa makini katika
kulinda amani na upendo wa nchi yetu kwani hii ndiyo nguzo kubwa katika
kipindi hiki," alisema.
Mhonda
pia alizungumza kuwa katika kutangazwa matokeo hayo pia ni vyema
matokeo hayo wananchi kuyakubali kwa moyo mmoja kwani kutokubali matokeo
kunaweza kuleta mkanganyiko wa amani.
Alisema
amani ya nchi ikilindwa itakuwa ni vyema hasa katika masuala ya kuleta
maenedeleo ya nchi hasa ukizingatia kuwa nchi inaenda kutafuta
maendeleo.
Akizungumzia
suala la kulinda kura Mhonda alisema kila chama kinatakiwa kuwaamini
mawakala ambao wamewaweka katika vituo na si kutaka kulinda nje.
"Watu
wanaosema kuwa kura zinatakiwa kulindwa watakuwa hawawaamini wale
mawakala ambao wanaweka katika vituo vya kuwapiga kura ili kusimamia
kura zao,"alisema.
Akizungumzia suala la mita 200 alisema hiyo ni sheria ambayo ipo katika tume ya uchaguzi hivyo haina budi kutekelezwa.
Mhonda
alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura
na kuchagua kiongozi bora ambaye atakuwa mstari wa mbele kupigania
maendeleo ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment