Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na.
Lilian Lundo – Maelezo
Serikali
kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetenga jumla ya Dola za Marekani Milioni
3.4 kusaidia vikundi vya wachimbaji wadogo na watoa huduma katika migodi nchini.
Akiongea
na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara ya Nishati na
Madini Badra Masoud amesema, hatua hii imekuja baada ya Serikali kubaini kwamba wachimbaji wengi
wadogo huchimba madini kwa kutumia zana na vifaa duni kutokana na ukosefu wa fedha za kununulia vifaa vya kisasa.
“Wachimbaji
wadogo wengi hawawezi kukidhi masharti ya kupata mikopo katika benki za
biashara nchini, hivyo Serikali inawajengea uwezo hatua kwa hatua hadi wafikie
hatua ya kuweza kukopesheka katika mabenki ya kibiashara,” alisema Badra.
Aidha,
Badra alisema kuwa pesa hizo zitatumika kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa
fedha 2015/16 kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji madini wadogo kupata ruzuku
kwa awamu ya tatu ili waweze kuchimba kisasa na kujiongezea vipato vyao na
kuongeza pato la Taifa.
Badra
alizidi kufafanua kwa kusema kuwa, ruzuku
hii ni jitihada za Serikali katika kukwamua wachimbaji wadogo kuondokana na
umasikini kwa kuwajengea uwezo wa
kufikia kuwa wachimbaji wa kati.
Vilevile
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imetenga maeneo yenye ukubwa wa
hekari 197,432 kwa ajili wa wachimbaji wadogo ili kuendeleza uchimbaji wa madini
mdogo nchini.
Serikali
itaendelea kuwa karibu na wachimbaji wadogo waliopatiwa ruzuku kuhakikisha
fedha wanazopewa wanazitumia kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo, wachimbaji
hao watapewa elimu ya uchimbaji wa kisasa, utunzaji wa mazingira na namna ya
kuepuka ajali ndani ya migodi
0 comments:
Post a Comment