Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokua akitoa
taarifa ya hali ya mfumuko wa bei Dar es Salaam,
kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira na Bei, Ruth Minja. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Story Na; Frank Shija, MAELEZO
Matumizi ya kaya kwenye biadhaa
za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia
47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa Bei umepungu
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu
mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.
Kwesigabo alisema kuwa kutokana
na mwenendo huo kunaashiria kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya
kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri,
mawasiliano, makazi, maji na nishati.
“Matokeo yanaonyesha kwamba
mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi
asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007” Alisema
Kwesigabo.
Aliongeza kuwa makundi mengi
mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya matumizi ya kaya mwaka
2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 mwaka
2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka
2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.
Aidha kumekuwa na ongezeko la
Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano
asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007
Kwa upande wake Meneja wa Takwimu
za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja
amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za Bei
zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na
mizania katikia bidhaa na huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri
,Maji na Nishati.
Aliongeza kuwa ili kupata matokeo
ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila
miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na
kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula
zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia
9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia
0.9.
Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa
kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na zimekuwa zikisaidia
katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya
kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa,kuboresha mishahara ya
wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi waliostaafu.
0 comments:
Post a Comment