Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 15 kuanzia leo kwa wakurugenzi wote
wa taasisi za serikali kupitia upya majina ya waajiriwa wao.
Dkt Magufuli amesema lengo la kufanya hivyo
ni kuondoa majina yote ya wafanyakazi ambao ni hewa ambao wanalipwa
fedha kila mwezi wakati kazi hawafanyi na hawapo katika maeneo yao ya
kazi.
''Mwezi uliopita tulilipa mishahara ya
wafanyakazi bilioni 500 mpaka 550 tukalipa na madeni ya nje bilioni 800
,katika malipo ya wafanyakazi wengi ni mishahara hewa na serikali
inalipa''.
''Sasa kuanzia leo wakurugenzi wote wapitie
majina ya wafanyakazi na ambao hawapo kazini wayaondoe majina hayo
haraka iwezekanavyo na wakurugenzi ambao hawatafanya hivyo ndani ya siku
15 watafukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani''
Aidha Rais Dkt Magufuli amewataka wakuu wa
mikoa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuwa tayari wamesaini kiapo cha
kutumikia wananchi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia sheria na taratibu
za utumishi wa umma.
0 comments:
Post a Comment