Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ni mdau wa masuala ya
kijamii nchini Bi. Maria Sarungi Tsehai amesema jitihada zinahitajika
zaidi hasa uwekezaji kwa elimu kwa watoto wa kike ili kuweza kufikia 50
kwa 50 mwaka 2030.
Bi
Sarungi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu siku ya
wanawake duniani siku ambayo kauli mbiu kwa mwaka huu inasema 50 KWA 50
mwaka 2030 Tuongeze Jitihada.
''Ili
kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ni lazima wadau wote kuunganisha
nguvu na kuhakikisha wanawake wanapata elimu na habari kuhusiana na
mambo mbalimbali yanayowahusu, kwa kuzingatia maeneo yote ya mijini na
vijijini''
Kwa
upande wa mila potofu kuhusu umiliki wa ardhi na usawa katika maeneo ya
kazi Bi Sarungi amesema kuna haja ya serikali na wadau kuangalia upya
suala la mishahara kwa upande wa wanawake kwani pamoja na shughuli
nyingi anazofanya mwanamke katika jamii mshahara wake katika kitengo
kimoja na mwanaume si sawa jambo ambalo linawarudisha nyuma wanawake.
Aidha
amepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na makamu wa Rais
mwanamke Mh Samia Suluhu ambaye Rais John Pombe Magufuli amemuamini na
kumtuma katika mikutano muhimu katika maeneo mbalimbali na kuonyesh
uwezo mkubwa katika uwakilishi huo.
Hivyo
amesisitiza kuwa wanawake wote ambao wamepata nafasi za uongozi katika
serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa uwezo wa hali ya juu ili iwe
chachu ya jamii kuthamini michango yao katika nafasi walizopewa.
0 comments:
Post a Comment